TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA PETER MADZANILE (31) RAIA NA MKAZI WA NCHINI ZIMBABWE AMEFARIKI DUNIA
PAPO HAPO BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI IT 6216 AINA YA TOYOTA
SPACIO ALIYOKUWA AKIENDESHA KUGONGANA NA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI STK
5988 AINA YA TOYOTA LAND CRUISER S/WAGON AMBULANCE MALI YA HALMASHAURI
YA WILAYA YA MBARALI ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA RASHID KAPOMBE (37)
MKAZI WA MBARALI.
TUKIO HILO LIMETOKEA KATIKA
BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE MNAMO TAREHE 13.07.2014 MAJIRA YA SAA 05:00
ALFAJIRI KATIKA KIJIJI CHA MAENGELE, KATA NA TARAFA YA ILONGO, WILAYA
YA MBARALI, MKOA WA MBEYA.
AIDHA KATIKA AJALI HIYO, DEREVA WA
GARI STK 5988, RASHID KAPOMBE PAMOJA NA ABIRIA WAKE DORAH MWASHILANGA
(32) MKAZI WA MBARALI WALIJERUHIWA NA WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA
MISHENI CHIMALA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA MAGARI YOTE MAWILI.
MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA NA MAJERUHI
WAMELAZWA HOSPITALINI HAPO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA
NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA
LA MAX SIMBEYE (60) MKAZI WA MAFIATI AMEFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA
KUFIKISHWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA MATIBABU BAADA YA KUGONGWA NA
GARI AMBALO HALIKUWEZA KUFAHAMIKA WALA DEREVA WAKE.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO
13.07.2014 MAJIRA YA SAA 12:30 MCHANA KATIKA ENEO LA MAFIATI, KATA YA
MANGA, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA, BARABARA YA
MBEYA/TUNDUMA. CHANZO CHA AJALI BADO KINACHUNGUZWA, DEREVA ALIKIMBIA NA
GARI MARA BAADA YA AJALI NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA
NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA
TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA
KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
KATIKA TUKIO LA TATU:
KATIKA TUKIO LA TATU:
MWANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA
KATIKA SHULE YA SEKONDARI IWAMBALA – UYOLE ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA
FROLA ASUKILE (14) MKAZI WA UYOLE AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA
KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.361 AQK AINA YA SUZUKI
ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE.
TUKIO HILO LIMETOKEA KATIKA
BARABARA YA MBEYA/TUKUYU MNAMO TAREHE 13.07.2014 MAJIRA YA SAA 17:45
JIONI KATIKA ENEO LA UYOLE YA KATI, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA,
JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI BADO KINACHUNGUZWA. DEREVA
ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA AJALI, JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA
NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA
TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA
KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
Imetolewa:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Imetolewa:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment