Lorietha Laurence na Rose Masaka(SJMC)
Serikali imeshauriiwa
kuendeleza mchakato wa kuhamishia ofisi zote zake mkoani Dodoma
kwenye makao makuu ya nchi yetu ili kuweza kupunguza msongamano wa watu
na magari.
Hayo yalisemwa na Mtanzania
Mzalendo, John Lyasenga wakati akizungumza na waandishi wa habari leo
katika ukumbi wa mikutano Idara ya Habari (MAELEZO) jijini Dar es
Salaam.
“ Kutokana na jiji la Dar es
Salaam kuwa na msongamano wa watu na foleni za magari, kuna umuhimu kwa
Serikali kufikiria suala hili la kuhamishia ofisi zake na huduma
zingine muhimu kwa mji huo mkuu wa Tanzania kwa ni kwa kufanya hivyo
kutaleta fursa kwa wakazi wa mji huo,”alisema Lyasenga.
Aidha aliongeza kuwa faida za
kuhamia Dodoma ni pamoja na kuwepo kwa fursa mbalimbali kama vile ajira
,kuongeza pato la mkoa kupitia ujenzi wa viwanda vitakavyoongeza
uzalishaji na kupunguza maafa kwa jiji la Dar es Salaam kama vile
mafuriko kutokana na wingi wa watu.
Mkoa wa Dodoma ina ukubwa wa
eneo 41,000 kilomita za mraba na idadi ya watu ni 2,083,588 kutokana na
Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012.
Aliongeza kuwa, hali ya hewa ya
mkoa huo ni nzuri,ukilinganisha na mkoa wa Dar es salaam wenye kilomita
za mraba 1,397 huku hali ya hewa, ikiwa ni joto wastani na idadi ya
watu ikizidi kuongezeka hadi kufikia milioni 4,364,541 sawa na
asilimia 4.3 kwa mwaka kutokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka
2012.
0 comments:
Post a Comment