Wednesday, 1 April 2015

Palestina yapewa uanachama wa ICC

Mahakama ya uhalifu wa kivita ICC
Wapalestina wamepata uanachama wa mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita miezi mitatu baada ya ombi lao kukubaliwa.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa Palestina Riad Malki anatarajiwa kutoa taarifa baada ya kuhudhuria sherehe za makaribisho kwenye mahakama hiyo mjini Hague.
Uanachama wa ICC unaiwezesha Palestina kuifungulia Israeli mashtaka ya uhalifu wa kivita lakini pia utachangia wanamgambo wa Hamas nao kufunguliwa mashtaka.
Serikali ya Palestina inasubiri kutoa malalamishi dhidi ya Israel kuhusu madai ya uhalifu wa kivita mnamo mwaka 2014 katika eneo la Gaza na hatua ya Israel kujenga makaazi katika ardhi yake.

0 comments: