Wednesday, 1 April 2015

TGNP YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI


 Mtafiti wa maswala ya kijamii kutoka Mtandaowa jinsia Tanzania(TGNP), Dinah Nkya,akitoa mada katika semina ya waandishi wa habari kutoka Kanda ya Nyanda za juu kusini.
 Afisa uhusiano wa TGNP, Melkizedeck Karol akiendesha mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari.
 Waraghibishi kutoka kituo cha maarifa na taarifa cha Tuamke, Nsalaga wakiwa kwenye chumba cha semina baada ya kutoa mambo mbali mbali waliyoyafumbua kutoka vijijini.
Waandishi wa habari wakishiriki semina hiyo.

 IMEELEZWA kuwa iwapo wanawake  wataendelea  kuwa  nyuma katika  kuwania nafasi mbali mbali za uongozi ikiwemo Urais bado changamoto  zilizopo katika jamii  zitaendelea  kuwatesa  wanawake nchini.
 
Kauli hiyo imetolewa  na ofisa mawasiliamo wa mtandeao wa Jinsia Tanzania(TGNP) Melikizedeck  Karol wakati  akitoa  mada ya  ushiriki  wa   wanawake  kwenye  uchaguzi  mkuu mwaka 2015 wakati  wa mafunzo ya siku  mbili ya  wanahabari  mikoa ya  nyanda  za  juu  kusini. Yaliyofanyika jijini Mbeya.
 
Alisema  kuwa  usawa  katika nafasi  za uongozi  wa  kutaka  kuwa na asilimia 50 kwa 50 kati ya  wanawake na  wanaume ni lazima  utimie  katika uchaguzi  huu  kwa  wanawake kuanza  kujitokeza kuwania nafasi  mbali mbali zikiwemo  za  juu kama Urais ,ubunge  na udiwani .
 
Hata hivyo Ofisa huyo alisema kwamba mwaka 2005  kuwa akidi nzima ya  bunge la jamhuri ya  muungano  wa Tanzania  ni wabunge 357 kwa  mujibu  wa katiba  hata  hivyo  viti maalum pekee ni 102 sawa na asilimia 28.6 vilivyogawanywa miongoni mwa vyama vya siasa kwa  kuzingatia  matokeo  ya uchaguzi kati ya  viti 239 vya majimbo (vikiwemo kutoka Zanzibar) ni wanawake 21 tu sawa na asilimia 8.8 ndio  walipewa viti  vya  kuchaguliwa bungeni.
 
 
Alisema ili kuwepo na usawa hakuna budi kwa wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi ikiwemo urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
 
"Hivi  wataka  kusema hakuna  mwanamke katika  nchi hii ambae  anaweza kuongeza nchini kama Rais na kama wapo  kwanini  hawajitokezi  kugombea nafasi za  juu kama Urais .....lazima  wanawake  wachangamkie nafasi  hiyo "
 
Alisema kwa mwaka 2005  kuwa akidi nzima ya  bunge la jamhuri ya  muungano  wa Tanzania  ni wabunge 357 kwa  mujibu  wa katiba  hata  hivyo  viti maalum pekee ni 102 sawa na asilimia 28.6 vilivyogawanywa miongoni mwa vyama vya siasa kwa  kuzingatia  matokeo  ya uchaguzi kati ya  viti 239 vya majimbo (vikiwemo kutoka Zanzibar) ni wanawake 21 tu sawa na asilimia 8.8 ndio  walipewa viti  vya  kuchaguliwa bungeni.
 
Huku  idadi  ya  madiwani  wa  kuchaguliwa  asilimia 4 na  wenyeviti wa  vijiji ni  asilimia 2 wakati  wenyeviti wa vitongoji ni asilimia 3 .
 
 Hivyo  alisema  ni  wajibu  kwa  vyombo  vya  habari na  wanawabari  nchini kuendelea kuhamasisha  makundi  ya  vijana na  wanawake  kujitokeza  kwa  wingi katika nafasi  za  udiwani ,ubunge na Urais katika  uchaguzi  mkuu mwaka huu.
 
Na Mbeya yetu Blog

 

0 comments: