Kampuni ya EAG Group Limited, imeingia mkataba wa miaka mitano na klabu
Simba kwa ajili ya kuitafutia mipango thabiti ya kuiendesha timu hiyo
kuhakikisha inapiga hatua katika maendeleo yake.
EAG Group iliingia mkataba na timu hiyo leo asubuhi kwenye hoteli ya
Southern Sun iliyopo Posta jijini Dar es Salaam.
Rais wa Simba, Evans Aveva alisema kuwa kwa
kumpitia udhamini wa kampuni hiyo wameandaa tuzo mbalimbali kwa wachezaji wao
kuhakikisha wanajituma uwanjani.
Aveva alizitaja tuzo hizo ni ya mchezaji bora wa mwaka atakayepewa gari
jipya, mchezaji kijana mwenye kipaji atkayepewa milioni 5 na mchezaji mwenye
nidhamu atakayeramba milioni moja.
Pia, wachezaji hao wote kila mmoja atapewa zawadi ya simu aina ya Huawei
yenye thamani ya shilingi milioni moja ambao nao wameingia kwenye udhamini huo.
“Lengo tunataka kuona timu yetu inapiga hatua katika soka ukanda wa
Afrika Mashariki na Afrika Mashariki na Kati na ndiyo tumetoa zawadi hizo kwa
ajili ya kuwapa morali wachezaji wetu kupitia Kampuni ya EAG Group Limited na
Huawei,” alisema Aveva.
Pia Mkurugenzi wa kampuni ya EAG Group, Imani Kajula alisema kuwa, huo ndiyo wa udhamini kwao, wamepanga kuleta mabadiliko ya soka kwa kuhakikisha wanawekeza zaidi kwa vijana kwa kuanza na Simba.
0 comments:
Post a Comment