CHELSEA YAMCHUKUA BEKI FILIPE LUIS TOKA ATLETICO MADRID
Mchezaji huyo mwenye Miaka 28 sasa atakwenda Stamford Bridge kwa upimwaji afya yake na kumalizana kuhusu maslahi yake binafsi.
Msimu uliopita, Luis alichezea Atletico
Mechi 44 na kuwasaidia kutwaa Ubingwa wa La Liga na kufika Fainali ya
UEFA CHAMPIONZ LIGI waliyopigwa 4-1 na Real Madrid.
Luis anakuwa Mchezaji wa Pili wa Atletico kusaini kuichezea Chelsea kufuatia Straika Diego Costa nae kujiunga.
Beki huyo, ambae amekuja kuchukua Namba
ya Ashley Cole aliekataliwa kuongezewa Mkataba na kutimkia AS Roma ya
Italy, alijiunga na Atletico Mwaka 2010 akitokea Deportivo La Coruna.
Luis ameichezea Brazil mara 4 na
aliwekwa kwenye Kikosi cha Akiba cha Brazil kwa ajili ya Fainali za
Kombe la Dunia zilizoisha hivi Juzi.
SASA BARCA YASEMA LUIS SUAREZ NI WAO!
Barcelona imesema Straika wa Liverpool Luis Suarez ni Mchezaji wao kwa Asilimia Mia Moja.
Wiki iliyopita Liverpool na Barca
zilikubaliana Dili ya Pauni Milioni 75 ya Uhamisho wa Mchezaji huyo
mwenye Miaka 27 kutoka Uruguay.
Lakini Barca hawaruhusiwi kumtambulisha
rasmi Mchezaji huyo kwa vile yuko kwenye Kifungo cha Miezi Minne
kutojihusisha na shughuli yeyote ya Kisoka baada kupatikana na hatia ya
kumuuma Meno Beki wa Italy Chiellini wakati wa Mechi ya Kombe la Dunia
kati ya Uruguay na Italy huko Brazil.
Amesema: “Tunawakubali Watu hapa na kasoro zao zote. Nina hakika atakuwa Mtu wa mchango mkubwa kwetu. Ni Mchezaji muhimu.”
DEMBA BA: BESIKTAS WAONGEA NA CHELSEA ILI KUMSAINI!
Klabu ya Uturuki Besiktas imetoboa kuwa ipo kwenye mazungumzo na Chelsea ili wamsaini Straika kutoka Senegal Demba Ba.
Ba, mwenye Miaka 29, alianza Mechi 23 kati ya 50 alizochezea Chelsea Msimu uliopita na kufunga Bao 14.
Kwenye Msimu huo, Ba alikuwa nyuma kwa namba akiwa chaguo la mwisho baada ya Samuel Eto'o na Fernando Torres.
Lakini Eto’o hivi sasa amemaliza Mkataba na Chelsea wamemsaini Diego Costa na hivyo Ba kuonekana hahitaji
0 comments:
Post a Comment