Van Gaal aliteuliwa kuwa Meneja wa Man United Mwezi Mei lakini muda wote huo alikuwa bado na kibarua chake na Timu ya Taifa ya Netherlands ambacho alikimaliza Jumamosi iliyopita baada ya kuifanikisha Nchi yake kutwaa Nafasi ya Tatu kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil.
Wachezaji wa Man United walirejea kwa ajili ya Mazoezi kabla Msimu mpya kuanza hapo Julai 4 wakiwa chini ya Meneja Msaidizi, Ryan Giggs.
Alhamisi Van Gaal atakuwa na mazungumzo na Wanahabari kuanzia Saa 11 Jioni Bongo Taimu.
Hii Leo huko Carrington, Van Gaal alipokewa na Ryan Giggs pamoja na Mtendaji Mkuu Ed Woodward na kisha kukutana na Wachezaji.
Van Gaal, ambae ametwaa Mataji ya Ubingwa akiwa na Klabu za Ajax, Barcelona, Bayern Munich na AZ Alkmaar, Ijumaa ataruka na Kikosi cha Man United kwenda kupiga Kambi huko California na kucheza Mechi yao ya kwanza hapo Julai 23 dhidi ya Los Angeles Galaxy.
VAN GAAL-Mataji yake:
-Ubingwa wa Ligi: Ajax (1993-94, 1994-95, 1995-96), Barcelona (1997-98, 1998-99), AZ Alkmaar (2008-09), Bayern Munich (2009-10)
-UEFA CHAMPIONZ LIGI: Ajax (1994-95)
-UEFA CUP: Ajax (1991-92)
Akiongelea ujio wa Van Gaal, Ed Woodward alisema wao wanaamini Meneja huyo ndie Mtu sahihi kumbadili David Moyes.
Ameeleza: “Bodi ipo nae kwenye mipango yake na kila Mtu anangojea kwa hamu Msimu mpya uanze. Historia yake ya kutwaa Ubingwa na Mataji Ulaya yote inamfanya awe Mtu sahihi hapa kwetu!”
USA-ZIARA YA KABLA MSIMU MPYA:
[Zote Nchini Marekani]
Manchester United v LA Galaxy
Chevrolet FC Cup
Jumatano 23 Julai 2014, Rose Bowl, Pasadena
Manchester United v AS Roma
International Champions Cup
Jumamosi 26 Julai 2014, Sports Authority Field, Denver
Manchester United v Inter Milan
International Champions Cup
Jumanne 29 Julai 2014, FedEx Field, Washington DC
Manchester United v Real Madrid
International Champions Cup
Jumamosi 2 Agosti 2014, Michigan Stadium, Ann Arbor
Manchester United v Valencia
REUNITED14
Jumanne 12 Agosti 2014, Old Trafford
0 comments:
Post a Comment