KIKOSI cha mabingwa wa Ligi ya Kenya, (KPL) Gor Mahia, kinawasili nchini kesho kwa ajili ya mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Simba, huku kiingilio cha chini katika mchezo huo kikiwa Sh.5000.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam leo, Makamu wa Rais wa
Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu' alisema kuwa maandalizi ya mchezo huo
yanaendelea kama yalivyoangwa.
Alisema wapinzani wao, watawasiri kesho mchana kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Kenya. Kaburu alisema licha ya kuwasili kwa Gor Mahia, wenyewe wao Simba nao watawasili siku hiyo hiyo, wakitokea Zanzibar.
|
Mshambuliaji tegemeo wa Gor Mahia, Dani Sserunkuma naye anakuja |
Alisema kuwa Gor Mahia imeomba ipate mechi mbili, hivyo siku ya Jumapili watakuwa na mchezo mwingine.
Alisema kwa upande wa Simba, kitarejea visiwani Zanzibar, kuendelea na ratiba zake nyingine za kambi ya kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kaburu alisema kuwa kunba mabadiliko yametokea na kufanya mchezo waliyoupanga awali, ambao ulikuwa dhidi ya Mtibwa Sugar, kubadilishwa. Alisema sababu kuu ya kufanya mabadiliko hayo ni maombi ya kocha wao Patrick Phiri, kuomba apate mechi ngumu, nao wakaamua kuwasiliana na timu hiyo kutoka Kenya.
Kaburu alisema kwa upande wa wanachama na wapenzi wa klabu ya Simba, watapata nafasi ya kuona timu yao, iliyokuwa imeweka kambi yake visiwani Zanzibar, ikiwa ni pamoja na kumuona kwa mara nyingine Mganda Emmanuel Okwi.
Alisema mchezaji huyo aliyesajiliwa Simba kwa mara nyingine, atakuwa amevaa jezi namba 25, ambayo alikuwa akiitumia kabla ya kuondoka Simba, kwenda Etoile du Sahel na baadae kwenda Yanga.
Pia Kaburu alisema kuwa viingilio vya mchezi huo, vvitakuwa sh.5000 kwa upande wa viti vya kijani, kwenye viti vya rangi ya chungwa itakuwa sh.10,000, huku VIP B na C, kikiwa sh.20,000 na VIP A kikiwa sh.30,000. Kaburu alisema tiketi za mchezo huo zitauzwa siku hiyo hiyo ya mechi kuanzia majira ya Saa 4:00 asubuhi.
Na Asha Said, DAR ES SALAAM
0 comments:
Post a Comment