ARGENTINA
imetinga fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuifunga Uholanzi kwa
penalti 4-2 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120 Uwanja
wa Sao Paulo nchini Brazil.
Sifa zimuendee kipa Sergio Romero aliyeokoa penalti mbili za Ron Vlaar na Wesley Sneijder na kuipeleka Argentina Fainali.
Arjen
Robben na Dirk Kuyt pekee ndiyo walifunga penalti upande wa Uholanzi,
wakati za Argentina zilikwamisha kimiani na Maxi Rodriguez, Sergio
Aguero, Ezequiel Garay na Lionel Messi.
Katika
mchezo huo uliochezeshwa na refa Cuneyt Cakir wa Uturuki, timu zote
zilishambuliana kwa zamu na sifa ziwaendee walinzi na makipa wa timu
hizo waliofanya kazi ya ziada kulinda nyavu.
Arjen
Robben alikuwa mwiba mbele ya safu ya ulinzi ya Argentina- kadhalika na
Lionel Messi alikuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya Uholanzi katika mchezo
huo wa marudio ya fainali ya mwaka 1978.
![]() |
Lionel Messi alifunga penali ya kwanza Argentina |
Shujaa wa matuta: Sergio Romero akiokoa penalti ya Ron Vlaar
Argentina sasa itamenyana na Ujerumani katika fainali ambayo jana iliwatoa wenyeji Brazil kwa mabao 7-1.
Kikosi
cha Uholanzi kilikuwa: Cillessen, De Vrij, Vlaar, Martins Indi/Janmaat
dk46, Kuyt, De Jong/Clasie dk62, Sneijder, Wijnaldum, Blind, Robben na
Van Persie/Huntelaar dk96.
Argentina:
Romero, Zabaleta, Demichelis, Garay, Rojo, Biglia, Mascherano,
Lavezzi/Maxi Rodriguez dk101, Messi, Perez/Palacio dk81 na
Higuain/Aguero dk82.
0 comments:
Post a Comment