KLABU
ya Liverpool iko mbioni kukamilisha usajili wa wachezaji wawili wa
kimataifa wa Ubelgiji kwa Pauni Milioni 30, Divock Origi na winga wa
Benfica, Lazar Markovic.
Origi
mwenye asili ya Kenya, aliyeichezea Ubelgiji Kombe la Dunia mwaka huu
Brazil, alipigwa picha wakati anawasili Liverpool Jumatano hii kujadili
vipengele vya Mkataba na viongozi wa Wekundu hao viwanja vya mazoezi vya
timu hiyo, Melwood na anaweza kwenda kufanyiwa vipimo Alhamisi hii
pamoja na Markovic.
Ada
ya Pauni Milioni 19.8 kwa ajili ya Markovic inaaminika imekubaliwa na
Benfica - wakati Origi ataondoka Lille ya Ufaransa kwa Pauni Milioni 10,
ingawa Tottenham nato imetupa ndoana zake kwa mshambuliaji huyo
Kibelgiji.
0 comments:
Post a Comment