Hivi karibuni kumekuwepo n
a
taarifa zilizoripotiwa na gazeti la Tanzania Daima la kila siku kuhusu
uwepo wa dawa zilizoisha muda wa matumizi kwenye duka la dawa la Core
Pharmacy jijini Dar es Salaam. Taarifa hizi zimekuwa zikitolewa na
mmiliki wa duka la dawa la Shine Care Pharmacy kwenye gazeti hilo.
Baadhi ya dawa zilizotajwa ni Listerine antiseptic mouthwash, Pimple
Gel, Misoprostol tablets 200mcg, Rabeloc IV 20mg, Mefenamic acidic
tablets, Herpex – 800 DT, Inhaler 100 pg dose, Metformin Denk 850,
Comprimes de carvediola 12.5mg na Cloderm cream.
Aidha, taarifa zimedai pia kuwa TFDA pamoja na kufahamishwa suala hili haikuweza kuchukua hatua zozote kwa mlalamikiwa.
TFDA inapenda kukanusha upotoshaji
huo unaofanywa na chombo hicho cha habari kutokana na ukweli uliopo.
TFDA ilifuatilia suala hilo na kubaini uuzwaji wa dawa moja tu ya
Listerine antiseptic mouthwash (chupa 2) ambayo iliuzwa katika kipindi
ambacho muda wake wa matumizi ulikuwa umebaki mwezi mmoja. Taarifa
zinazoendelea kutolewa na gazeti la Tanzania Daima zinatokana na mgogoro
uliopo baina ya makampuni mawili ya kuuza dawa ya Core Pharmacy na
Shine Care Pharmacy.
TFDA inauhakikishia umma kwamba
iko makini na ina mifumo madhubuti ya kufuatilia ubora, usalama na
ufanisi wa dawa, chakula, vipodozi na vifaa tiba kwenye soko. TFDA
inaviasa vyombo vya habari pia kufanya uchunguzi wa kina na kufika
ofisini kwake ili kupata taarifa sahihi badala ya kutoa taarifa
inazozipokea kutoka kwa wafanyabiashara.
Imetolewa na:-
MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA
EPI MABIBO EXTERNAL,
S.L.P 77150, DAR ES SALAAM
Simu: + 255 222 450512/450751/452108
Nukushi: + 255 222 450793
Barua pepe: info@tfda.or.tz
Tovuti: www.tfda.or.tz
0 comments:
Post a Comment