Kocha mkuu wa JKT Ruvu, Fredy Felix Minziro ( wa kwanza kushoto) akiwa kazini msimu ulipita wa ligi kuu soka Tanzania bara
MAAFANDE wa JKT Ruvu Stars wametamba kufanya
vizuri katika michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara inayotarajia kuanza
kushika kasi septemba 20 mwaka huu.
Kocha mkuu wa klabu hiyo, Fredy Felix Minziro
ameuambia mtandao huu kuwa timu yao
ilikuwa imeanza mazoezi na vijana au chipukizi na baadaye wakaanza na wa zamani.
Minziro aliongeza kuwa vijana hao wamewasajili kutoka
katika mpango maalum wa kusaka vipaji ambao klabu iliuendesha kwa kualika
vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini kufanya majaribio klabuni hapo.
“Kwa ujumla suala la usajili limeenda vizuri kwa maana
ya vijana wengi tuliowapa, kwa kiwango fulani wanaridhisha na ambao
hawaridhishi tunawatoa. Naamini kwa vijana tunaowapa na kuwasajili tutakuwa na
timu nzuri”.
“Nafahamu kuwa ligi itakuwa na ushindani mkubwa
kutokana timu zilizopanda, lakini naamini vinaja tutakaowasajili watatusaidia.
Nitafanya kazi ya ziada kwasababu timu yote ni mpya na baadhi ya wachezaji wa
zamani tumewaondoa”.
Hata hivyo, Minziro alisema anahitaji kupata
wachezaji wenye uzoefu katika kikosi chake, lakini wasiwe wengi zaidi kwasababu
kuna wengine ameamua kuwabakisha.
“Ni kweli wachezaji wenye uzoefu wanahitajika,
lakini wasiwe wengi, kwa maana ya kwamba uwachanganye na vijana. Kama
nilivyokuambia, baadhi yao tumewapunguza, lakini wakonggwe nanaowataka inategemeana
kidogo ni umri upi”.
Fredy
Felix Minziro alibebwa na mchezaji wake baada ya JKT Ruvu kuifunga
Simba mabao 3-2 msimu uliopita ndani ya uwanja wa Taifa.
“Kama unavyojua wachezaji wengi wa JKT Ruvu
wamekaa na timu kwa muda mrefu, kwahiyo wengine tumeamua kuwapumzisha na
wengine tumewaacha ili tuwachanganye na damu changa”.
Tanzania haina mfumo sahihi wa soka la vijana,
hivyo wachezaji wengi wanakosa misingi ya mpira, lakini Minziro alisema
atajitahidi kuhakikisha anawajenga vizuri na watakuwa na kiwango cha juu.
“Ni kweli,
vijana wengi hawana misingi ya mpira kutoka chini, lakini ukiwa kama
kocha lazima ufanye kazi ya zaida kwa maana ya kwamba, yale mambo ambayo hawayaelewi, unaendelea
kuyasisitiza na kuyafanyia kazi mpaka watakapokaa sawa. Kikubwa ambacho
nakazania katika mazoezi yangu ni kuwaimarisha mwili na kuwapatia misingi ya
mpira”. Alisema Minziro.
Pia kocha huyo amefurahishwa na kitendo cha
shirikisho la soka Tanzania, TFF, kusogeza ligi kwa takribani mwezi mzima tangu
tarehe ya awali iliyotangazwa ambayo ilikuwa Aosti 24 mwaka huu mpaka septemba
20.
“Kwangu mimi nimefurahishwa sana na TFF kusogeza
ligi mbele, kwasababu unafahamu kwamba kuna wachezaji karibu 10 hawapo katika
kikosi cha timu yangu. Wapo kwenye timu ile ya `kombaini` ya majeshi, sasa
nilikuwa napata matatizo makubwa sana, timu ni mpya, halafu na wengine 10
hawapo, sasa utafanya mazoezi ya aina gani ndugu yangu?
“Kwahiyo kusogeza mbele, nadhani itakuwa nzuri. Nadhani majeshi watamalrza mashindano yao Agosti 27, kwahiyo nitawapata vijana wangu na nitakuwa nao pamoja angalau kwa wiki mbili kabla ya kuanza ligi kuu”. Aliongeza Minziro.
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
0 comments:
Post a Comment