Tottenham Hotspurs wamefanikiwa kuwafunga Arsenal katika mchezo wa ligi kuu ya England uliopigwa hii leo (Jumamosi) kwenye uwanja wa White Hart Lane ukiwa mchezo wa kwanza wa ligi hiyo kwa ratiba ya jumamosi .
Arsenal ndio walianza mchezo huo kwa kasi zaidi wakipata bao la kwanza kupitia kwa kiungo mshambuliaji Mesut Ozil ambaye alifunga kwenye dakika ya 11 .
Spurs walisawazisha bao hilo kupitia kwa mshambuliaji chipukizi Harry Kane ambaye alifunga kwenye dakika ya 56 ya mchezo zikiwa zimepita dakika 9 tangu kuanza kwanza kipindi cha pili .
Kane aliwahakikishia Tottenham pointi zote tatu kwenye dakika ya 86 kwa kufunga bao la pili bao ambalo limewapaisha Spurs mpaka kwenye nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi kuu ya England.
Kane hadi sasa amefunga mabao 12 kwenye ligi hiyo ambapo anashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa wafungaji akiwa nyuma ya Diego Costa , Sergio Aguerro na Charlie Austin .
CHELSEA YAPAA POINTI 7 MBELE YA MAN CITY
RATIBA/MATOKEO:
**Saa za Bongo
Jumamosi Februari 7
Tottenham 2 Arsenal 1
Aston Villa 1 Chelsea 2
Leicester 0 Crystal Palace 2
Man City 1 Hull City 1
QPR 0 Southampton 1
Swansea 1 Sunderland 1
2030 Everton v Liverpool
MABINGWA WATETEZI wa Ligi Kuu England, Manchester City, Leo hii wakiwa kwao Etihad wametoka Sare na Hull City na kuwaruhusu Vinara Chelsea kuongoza Ligi wakiwa Pointi 7 mbele yao baada ya kushinda Ugenini Bao 2-1 dhidi ya Aston Villa.
City walinusurika kufungwa na Hull City walioongoza kwa Bao la Dakika ya 35 la David Meyler na kusawazisha Dakika ya 90 kwa Bao la James Milner.
Chelsea, wakicheza Ugenini Villa Park, walifunga Bao la Kwanza Dakika ya 8 kupitia Eden Hazard na Villa kurudisha Dakika ya 48 kupitia Jores Okore lakini ni Branislav Ivanovic, kwenye Dakika ya 66, ndie aliewapa ushindi kwa kufunga Bao safi kwa kigongo.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumapili Februari 8
1500 Burnley v West Brom
1705 Newcastle v Stoke
1915 West Ham v Man United
Jumanne Februari 10
2245 Arsenal v Leicester
2245 Hull v Aston Villa
2245 Sunderland v QPR
2300 Liverpool v Tottenham
Jumatano Februari 11
2245 Chelsea v Everton
2245 Man United v Burnley
2245 Southampton v West Ham
2245 Stoke v Man City
2300 Crystal Palace v Newcastle
2300 West Brom v Swansea
MSIMAMO:
0 comments:
Post a Comment