Waziri wa elimu Liberia, Etmonia Tarpeh
ametangaza kufunguliwa kwa Shule zilizokuwa zimefungwa kwa zaidi ya
miezi sita nchini humo kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
Ufunguzi huo ulipangwa kufanyika
February 2, lakini ulisogezwa mbele ili kupata nafasi ya kusambaza vifaa
vya kutosha kwa ajili ya kufanyia usafi wa mazingira na vifaa
vingine kwa shule za Serikali na binafsi.
Idadi
ya wanafunzi walioripoti mashuleni siku ya jana February 16 imepungua,
ili kuhakikisha usalama wa watoto hao michezo imepigwa marufuku ili
kuepuka kugusana, pia vimechapishwa vipeperushi vya usalama
vinavyowaonesha watoto hao jinsi ya kujilinda na maambukizi.
Shirika
la Afya duniani (WHO) limesema idadi ya watu waliofariki kwa Ebola
Liberia ni 3,800 tangu ulipotiwe kulipuka December 2013.
0 comments:
Post a Comment