Monday, 12 October 2015

Raia wa China aliyekamatwa kwa makosa ya ulanguzi wa pembe za ndovu anyimwa dhamana na mahakama

 

Image copyright
Image captionMalkia wa pembe za ndovu kusalia korokoroni TZ
Mwanamke mmoja raia wa China aliyekamatwa kwa makosa ya ulanguzi wa pembe za ndovu zenye thamani ya dola milioni mbili u nusu amenyimwa dhamana na mahakama moja hapa Dar es Salaam.
Upande wa mashtaka umedai kuwa bi Yang Feng Glan ndiye aliyekuwa akisimamia njama yote ya usafirishaji wa pembe za ndovu kinyume cha sheria mbali na makosa mengine ya uhalifu.
Kimsingi bi Feng Glan ndiye aliyekuwa bosi katika genge la majambazi walioshiriki uwindaji haramu na matukio mengine ya wizi wa kupangwa wa kimabavu.
Wachunguzi wameishawishi mahakama kuwa japo bi Yang Feng Glan anasifika kwa kuendesha kwa ufanisi biashara ya mikahawa na ukulima lakini pia ni mvunjaji mkubwa wa sheria.
Utawala hapa Tanzania umempa bibi huyu hadhi ya 'Malkia wa pembe za ndovu'' baada ya kuchunguza na kufwatilia nyendo zake kwa zaidi ya mwaka mmoja katika uchunguzi uliokamilika alipokamatwa jijini
Dar es Salaam juma lililopita.
Vyombo vya dola hapa vinadai kuwa Feng Glan ndiye mfadhili mkuu wa uwindaji haramu wa ndovu mbali na ulanguzi wa wa zaidi ya pembe 700 za ndovu katika kipindi cha miaka 14.
Mashirika yanayopigania uhifadhi wa mazingira na wanyama pori nchini Tanzania wamefurahishwa na hatua ya serikali kumchukulia hatua mchina huyo.
Image copyrightGetty
Image captionTanzania ilipoteza thuluthi mbili ya ndovu wake katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.
Mashirika hayo hata hivyo yanasema sharti Feng Glan aukabili mkono wa sheria ili iwe mfano kwa wahusika wengine wa biashara hiyo mbaya ya uwindaji haramu kwa ustawi wa wanyama pori.
Mwaka uliopita shirika moja la uhifadhi wa mazingira na wanyama pori lenye makao yake nchini Uingereza (Environmental Investigation Agency) lilichapisha ripoti ya utafiti iliyoonyesha kuwa Tanzania ilipoteza thuluthi mbili ya ndovu wake katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.
katika kipindi hichi uchunguzi ulidai mahakamani kuwa bibi Feng alikuwa akiendesha genge la wawindaji haramu.
Iwapo atapatikana na hatia bi Feng anakabiliwa na hukumu ya miaka 30

0 comments: