
Kocha mkuu wa Yanga sc, Marcio Maximo (kulia) akiwa na msaidizi wake Leonardo Neiva (kushoto).
UJIO wa Marcio Maximo katika klabu ya Yang sc
umemvutia beki na kocha wa zamani wa klabu hiyo, Fred Felix Minziro ambaye
kwasasa ni kocha mkuu wa JKT Ruvu ya Pwani.
Akizungumza na MPENJA BLOG, Minziro amesema yeye
falsafa yake ni kucheza soka la kuvutia, hivyo anaamini atakuwa mpinzani mkubwa
wa Maximo.
“Hakuna asiyefahamu kwamba soka langu ni la
kuvutia, hakuna asiyefahamu hilo. Na naamini hata kama timu inanifunga, kila
mtu anatoka uwanjani akiwa amaridhika . Nahakikisha kwamba soka hili linarudi
tena ndani ya JKT, ingawa mwaka huu lisiwe zuri sana, lakini mwakani litakuwa
bora zaidi”.

Kuhusu ujio wa Maximo katika klabu ya Yanga,
Minziro alisema amefurahishwa sana kwasababu kocha huyo analijua soka la
Tanzania na utamaduni wake.
“Mimi nasema ni vizuri, ujio wa Maximo nimeufurahia
sana, mkazo ni kwa viongozi wa Yanga. Unajua viongozi wa Yanga mara nyingi
wamekuwa sio wakweli, unaweza kuwaambia unahitaji hiki na hiki na wasikutimizie”.
“Lakini kwa Maximo ninvyomfahamu mimi, ni kocha
mwenye msimamo. Nadhani viongozi watafika muafaka na kuteleleza matakwa yake”. Alisema
Minziro.
Ujio wa Maximo ni changgamoto nzuri kwangu,
kwasababu naamini timu ya JKT Ruvu itakutana na kocha huyo katika ligi, itakuwa
ni mechi nzuri.Pambano litakuwa zuri sana”.
“Pia kwa upande wa viongozi, nadhani Maximo
atawasukuma na kuhakikisha Dar Young Africans wanajenga uwanja mzuri wa
mazoezi, nadhani wakati tukiwa na Brandts tulikuwa tunalalamika uwanja wa
mazoezi”.
“Naamini Maximo atawabadilisha viongozi wa Yanga, watabadilika, wataenda kwa mtindo wa kisasa na kuacha kwenda kizamani”. Alihitimisha Minziro mwenye mapenzi na Yanga sc.
Na Baraka Mpenja Dar es salaam
0 comments:
Post a Comment