LIONEL Messi amepoza machungu kidogo baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Kombe la Dunia 2014.
Nyota huyo wa Barcelona ameshindwa kuisaidia Argentina kutwaa Kombe la Dunia baada ya kufungwa 1-0 na Ujerumani katika Fainali
Uwanja wa Maracana mjini Rio de Jeneiro, Brazil.
Bao
hilo pekee la Ujerumani, lilifungwa na Mario Gotze aliyeingia kuchukua
nafasi ya Miroslav Klose dakika 88, aliyefunga bao hilo pekee dakika ya
112.
Mlinda mlango wa Ujerumani, Manuel Neuer ameshinda tuzo ya kipa bora wa
mashindano ya mwaka huu, ambayo wenyeji Brazil wameambulia nafasi ya nne
baada ya kufungwa 3-0 na Uholanzi jana, kufuatia kutolewa na Ujerumani
kwa kipigo cha mabao 7-1 katika Nusu Fainali.
James
Rodriguez wa Colombia amekuwa mfungaji bora kwa mabao yake sita, licha
ya timu yake kutolewa Robo Fainali. Amefuatiwa na Thomas Muller wa
Ujerumani mabao matano, Lionel Messi mabao manne sawa na Robin van
Persie wa Uholanzi.

0 comments:
Post a Comment