Na Rose Masaka
MAELEZO
Dar es Salaam
KITUO cha kulea watoto yatima New
Hope Family Group (NHFG) kilichopo Kata ya Mji Mwema Kigamboni Wilaya ya
Temeke Jijini Dar es Salaam kinahitaji kiasi cha Tsh. Milioni 120 kwa
ajili ya kukamilisha ujenzi wa makazi ya watoto katika eneo la Mwasonga
Kata ya Kisarawe II.
Katika kufanikisha lengo hilo, Kituo hicho kimeandaa futari maalum tarehe 18. Julai, 2014 sawa na mfungo 20 wa mwezi wa Ramadhani itakayoongozwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar wa Salaam Alhad Musa Salum kama sehemu ya harambee ya kukusanya fedha hizo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Ijumaa (Julai 11, 2014), Katibu Mtendaji wa kamati ya Maandalizi, Bw. Azizi Mchele alisema tatizo la ongezeko la watoto wa mitaani nchini ni suala mtambuka linalomgusa kila mwanajamii kwa nafasi aliyopo. Akifafanua zaidi alisema kituo hicho kinahitaji matofali 10,000, saruji mifuko 1000, kokoto na mchanga vyenye thamani ya Tsh. Milioni 5, mbao za nyumba zenye thamani ya Tsh. Milioni 1, mabati 100 yenye thamanni ya Tsh. Milioni 1.8, nondo za kujengea uzio 400 zenye thamani ya Tsh. Milioni 6.4. Aidha Mchele aliongeza kuwa mahitaji mengine ni pamoja na ndoo za rangi 50 zenye thamani ya Tsh Milioni 1.4, vitanda vya kulalia 60 vyenye thamani ya Tsh. 16.8, magodoro 100 yenye thamani ya Tsh. Milioni 4.8, mashuka 160 yenye thamani ya Tsh. Milioni 1.3 pamoja na mito 180 yenye thamani ya Tsh. Laki 4.5. Mchele alisema mpaka kufikia sasa kituo hicho kimefanikiwa kujenga nyumba tatu, ikiwemo nyumba mbili (2) za kulala na bwalo la chakula, pamoja na ujenzi wa vyoo vinane (8), ambapo vyote kwa pamoja ujenzi huo uligharimu kiasi cha Tsh. Milioni 54. “Fedha hizi zimetokana na nguvu zetu wenyewe pamoja na michango ya wahisani mbalimbali. Bado tuna changamoto ya jingo moja kwa ajili ya walimu (walezi), pamoja na uzio” alisema Mchele. Aliongeza kuwa kituo hicho pia kimefanikiwa kusomesha watoto wote 45 inayowalea katika kituo hicho, ikiwemo wanafunzi 7 waliopo katika shule mbalimbali za sekondari, ambazo ni Aboud Jumbe, Kisota na Kidete zilizopo katika Kata ya Kigamboni Wilayani Temeke. Kwa upande wake Mama Mlezi wa Kituo hicho, Bi. Merry Stromberg alisema ili kukabiliana na tatizo la ongezeko la watoto wa mitaani nchini, Serikali na sekta binafsi hazina budi kuunganisha nguvu za pamoja kwani kwa sasa tatizo hilo limeshindwa kupatikana mwafaka wake.

0 comments:
Post a Comment