UFARANSA, mabingwa wa mwaka 1998 wapo kundi moja na Uswisi, Ecuador na Honduras katika Kombe la Dunia mwaka huu.
BIN ZUBEIRY inaendelea kukuletea makala za mchambuzi na beki wa zamani wa England, Martin Keown hapa akilichambua Kundi E.
Kundi E
Ufaransa
Ecuador
Honduras
Uswisi
Utabiri wa Keown;
1 Ufaransa
2 Usiwsi
3 Honduras
4 Ecuador
Ratiba (Saa za Afrika Mashariki)
Jun 15 Usiwsi v Ecuador Saa 1:00 usiku Brasilia
Jun 15 Ufaransa v Honduras Saa 4:00 usiku P. Alegre
Jun 20 Uswisi v Ufaransa Saa 4:00 usiku Salvador
Jun 20 Honduras v Ecuador Saa 7:00 usiku Curitiba
Jun 25 Honduras v Uswisi Saa 5:00 usiku Manaus
Jun 25 Ecuador v Ufaransa Saa 5:00 usiku R. Janeiro
Jun 15 Ufaransa v Honduras Saa 4:00 usiku P. Alegre
Jun 20 Uswisi v Ufaransa Saa 4:00 usiku Salvador
Jun 20 Honduras v Ecuador Saa 7:00 usiku Curitiba
Jun 25 Honduras v Uswisi Saa 5:00 usiku Manaus
Jun 25 Ecuador v Ufaransa Saa 5:00 usiku R. Janeiro
USWISI
Viwango vya FIFA: Namba 6
Kocha: Ottmar Hitzfeld. Baada ya miaka zaidi ya 30 ya kufundisha mpira, Mjerumani huyo atastaafu baada ya Kombe la Dunia.
Nahodha: Gokhan Inler (Napoli)
Mchezaji wa kumulikwa: Granit
Xhaka (Borussia Monchengladbach). Na alivyo na mwili mkubwa ni kama
lilivyo jina lake. Ana umri wa miaka 21 tu, lakini tayari kiungo
ameichezea timu yake ya taifa mechi 22, ana uwezo mkubwa wa kupitia
mipira miguuni mwa wapinzani na kuipandisha timu haraka kushambulia.
Nakuja kwako? Xherdan Shaqiri wa Uswisi amekuwa akihusishwa na kuhamia England
Ubora wao: Wazee
wa maajabu. Wakiwa na ukuta wa nguvu na mfumo wa kutengeneza
mashambulizi ya kushitikiza walifanikiwa kumaliza wimbi la Hispania
kushinda mechi 11 mfululizo katika Fainali zilizopita za Kombe la Dunia
na kuifunga Brazil 1-0 Agosti mwaka jana.
Hatari: Kutafuta
mfungaji wa mabao. Mfungaji wao bora katika mechi za kufuzu alikuwa
beki wa FC Basle, Fabian Schar aliyefunga mabao matatu. Hii si sawasawa
kuelekea Kombe la Dunia.
Watakwenda England? Xherdan
Shaqiri yumo katika orodha ya wachezaji wanaotakiwa Liverpool na
amekubali kuondoka Bayern Munich iwapo atapata nafasi zaidi ya kucheza.
Beki Schar anatakiwa na Tottenham.
Matokeo mazuri Kombe la Dunia: Robo Fainali (1934, 1938 na 1954)
Walivyofika hapa: Waliongoza kundi
lao bila kupoteza mechi, japokuwa walipangwa pamoja na Iceland,
Slovenia, Norway, Albania na Cyprus haikuwa kazi ngumu kwao.
Je, wajua? Wachezaji 13 katika kikosi cha Uswisi wangeweza kuchezea nchi nyingine.
ECUADOR
Viwango vya FIFA: Namba 26
Kocha: Reinaldo Rueda. Pamoja na kuwa kocha wa soka, Mcolombia huyo pia ni Profesa wa Chuo kikuu.
Nahodha: Antonio Valencia (Manchester United)
Mchezaji wa kumulikwa: Felipe
Caicedo (Al Jazira). Valencia ndiye anayefahamika zaidi, lakini Caicedo
ni tegemeo lao la mabao. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City
ana nguvu, mtaaoamu na alikuwa mfungaji bora katika mechi za kufuzu.
Antonio
Valencia (kulia) alipewa kadi nyekundu katika mechi ya kirafiki Ecuador
ikitoka sare na England baada ya kugombana na Rahim Sterling
Ubora wao: Wanacheza
kitimu. Mshambuliaji Christian Benitez alifariki dunia katikati ya
mechi za kufuzu, lakini kama timu, waliunganisha nguvu zao na kucheza
hadi kufuzu, ushindi wa 1-0 dhidi ya Uruguay ndiyo uliowavusha.
Hatari: Ukuta
wa ufa. Wana washambuliaji wengi wenye vipaji, lakini wanakosa mabeki
imara – wamecheza mechi mbili tu bila nyavu zao kutikiswa kati ya
michezo 10.
Watakwenda England? Watford
inamtaka beki wa pembeni Juan Carlos Paredes, wakati Swansea, West Ham,
Wigan na Cardiff zinagombea saini ya iwnga mwenye kipaji Jefferson
Montero.
Matokeo mazuri Kombe la Dunia: 16 Bora (2006)
Walivyofika hapa: Walishika
nafasi ya nne na ya mwisho ya kufuzu kwa Amerika Kusini, lakini
iliwapiku Uruguay kwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Je, wajua: Kocha Rueda amewahi kufika Kombe la Dunia kabla, lakini kama kocha wa wapinzani wake katika Kundi E, Honduras mwaka 2010.
UFARANSA
Viwango vya FIFA: Namba 17
Kocha: Didier Deschamps. Ameitwa ‘mbeba maji’ na Eric Cantona, lakini ushindi unaweza kuongeza heshima ya gwiji huyo.
Nahodha: Hugo Lloris (Tottenham)
Mchezaji wa kumulikwa: Paul
Pogba (Juventus). Manchester United watajilaumu wenyewe kwa kumruhusu
Pogba kuondoka. Kiungo huyo chipukizi ni mahiri, anakimbia na alikuwa
nyota Juventus wakitwaa ubingwa Serie A.
Jaribio la Ufaransa: Kiungo Paul Pogba ametabiriwa kung'ara Kombe la Dunia akiwa na Les Bleus
Ubora wao: Kutawala
sehemu ya kiungo. Ufaransa ina vipaji vingi na Deschamps ameonyesha
wepesi kwa kuamia kuhamia kutoka mfumo wa 4-2-3-1 na kutumia mfumo wa
kushambulia zaidi wa 4-3-3.
Hatari: Kuzorota.
Tangu watwae Kombe la Dunia nyumbani mwaka 1998, Ufaransa imekuwa
ikivurunda katika mashindano mengi yaliyofuatia na kushuka kwa thamani
yao.
Watakwenda England? Nyota
wa Porto, Eliaquim Mangala yuko njiani kutua Chelsea ingawa pia
Manchester City nap wanamtaka. Antoine Griezmann anatakiwa na Arsenal na
Liverpool.
Matokeo mazuri Kombe la Dunia: Washindi (1998)
Walivyofika hapa: Walishika
nafasi ya pili kwenye kundi lao nyuma ya Hispania na walilazimika
kukipikua kipigo cha mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza wa kufuzu dhidi
ya Ukraine. Ushindi wa 3-0 nyumbani uliwapa tiketi ya Brazil.
Je, wajua? Deschamps
atakuwa mtu wa pili tu kutwaa Kombe la Dunia kama Nahodha na kama kocha
baada ya Franz Beckenbauer. Mario Zagallo wa Brazil ameshinda pia Kombe
hilo kama mchezaji na kocha, lakini Nahodha wa nchi yake.
HONDURAS
Viwango vya FIFA: Namba 33
Kocha: Luis Fernando Suarez
Nahodha: Noel Valladares (Olimpia)
Mchezaji wa kumulikwa: Carlo
Costly (Real Espana). Ni hatari mno anapokuwa karibu na lango na
mchezaji huyo wa Honduras mwenye urefu wa futi 6 na inch 3 ni tishio kwa
mabeki. Anafunga mabao muhimu na anacheza kwa moyo.
Ubora wao: Hawana
makuu. Bila kuwa na nyota yeyote mkubwa, Honduras wanatumia mfumo wa
kigumu wa 4-4-2 wakicheza na viungo wakabaji wawili na mawinga wenye
kasi kumlisha mipira mtu wao wa mwisho.
Tatizo: Kufunga mabao. Hawakufunga bao Fainali za mwaka 2010 na mara ya mwisho kufunga kwenye Kombe la Dunia ilikuwa mwaka 1982.
Atakwenda England? Sehemu ya wachezaji wake bora tayari wanacheza England, lakini winga wa Anderlecht, Andy Najar anatakiwa na Hull na Tottenham.
Matokeo mazuri Kombe la Dunia: Hatua ya Makundi (1982 na 2010)
Walivyofika hapa: Waliongoza
kundi lao katika hatua ya kwanza ya kufuzu kabla ya kushika nafasi ya
tatu katika hatua ya pili na ya mwisho ya kufuzu, nyuma ya Marekani
na Costa Rica hivyo kujikatia tiketi ya Brazil.
Je, wajua? Baada
ya Honduras kufuzu Kombe la Dunia, Rais Pepe Lobo alitangaza siku ya
mapunziko kitaifa. Pia anafikiria kumpa kila raia mapumziko ya siku
kuangalia mechi za Honduras.
0 comments:
Post a Comment