
Nicola Rizzoli
amechaguliwa na Fifa kuwa mwamuzi katika mchezo wa fainali - Kombe la Dunia
Brazil 2014 kati ya Ujerumani na Argentina.
Howard Webb kutoka
England, aliyechezesha fainali ya Kombe la Dunia 2010 Afrika Kusini,
aliorodheshwa lakini hakuchaguliwa.
Ujerumani
itapambana na Argentina kwenye dimba la Maracanã, jijini Rio De Janeiro, siku
ya Jumapili Julai 13.
Rizzoli ni msanifu
majengo kutoka Bologna, na tayari amechezesha mechi tatu katika michuano ya Kombe la Dunia Brazil.
Mwamuzi huyo mwenye umri wa miaka 42 alichezesha
mechi kati ya Spain dhidi ya Uholanzi, Nigeria na Argentina na Argentina
ilipocheza na Ubelgiji.
Rizzoli pia alichezesha mchezo wa fainali ya Ligi
ya Europa kati ya Atlètico Madrid dhidi ya Fulham mwaka 2010, na pia mchezo wa
fainali ya Uefa Klabu Bingwa Ulaya mwaka 2013 kati ya Bayern Munich na Borussia
Dortmund.
Rizzoli atasaidiwa na waamuzi wa pembeni Renato
Faverani na Andrea Stefani, na mwamuzi wa nne atakuwa Carlos Vera kutoka
Ecuador.
Rizzoli atakuwa mwamuzi wa tatu kutoka Italy
kuchezesha fainali, baada ya Sergio Ginella mwaka 1978 na Pierluigi Collina
mwaka 2002.
0 comments:
Post a Comment