BEKI
Mathieu Debuchy yuko mbioni kukamilisha uhamisho wake wa Pauni Milioni
11 kutua Arsenal akitoka kwa wapinzani wa Ligi Kuu ya England,
Newcastle.
Beki
huyo wa kulia wa Ufaransa amekuwa akihusishwa na kuhamia The Gunners
kwa wiki kadhaa sasa na sasa anatarajiwa kusaini baada ya Fainali za
Kombe la Dunia.
Ufaransa
ilitolewa katika Robo Fainali na Ujerumani na Debuchy amerejea England
kukamilisha vipimo vya afya na The Gunners Jumatatu.
Uamuzi wa Arsenal kumfuata Debuchy unafuatia kuondoka kwa Bacary Sagna anayehamia Manchester City kama mchezaji huru.
Debuchy alikuwa anaanzishwa mbele ya Sagna katika kikosi cha Ufaransa kwenye Kombe la Dunia. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ameichezea mechi 46 Newcastle, akiifungia bao moja tu - dhidi ya wapinzani Sunderland.
Alisajiliwa
kutoka Lille ya Ufaransa kwa Pauni Milioni 5.5 Januari mwaka 2013
na Newcastle sasa inataka kumsajili ama Micah Richards wa Manchester
City au Carl Jenkinson wa Arsenal wazibe pengo la kisiki hicho.
0 comments:
Post a Comment