UNAFIKI na USALITI wa Mwigamba dhidi ya tuhuma za ukomo madaraka katiba ya CHADEMA.
Nimeamua
kuandika kidogo kikombe kisinipite ili kuanika unafiki wa Mwigamba na
marafiki zake (Kitila na Zitto), Mwigamba na maswahiba zake (viruka njia
wa usaliti) ambao walisaliti ndani ya CHADEMA na baadae kuibuka na
uzushi kuwa kipengele cha 6.3.2 (c) kinacho zungumzia muda wa uongozi
kwenye katiba ya chama kuwa kimewekwa kinyemela. Kipengele hicho (6.3.2
(c), kinasema "kiongozi aliye maliza muda wa uongozi ana haki ya
kugombea na kuchaguliwa tena mradi awe anatimiza masharti ya kuchaguliwa
kuwa kiongozi"
Mwigamba anasema kipengele hicho kimeongezwa
kinyemela huku akijua alishiriki/wameshiriki kwenye kuifanyia mabadiliko
katiba ya chama ya 2004 na kuanza kutumika rasmi kwa katiba ya 2006
iliyokuja na kipengele hicho.
Mwigamba
pamoja na wajumbe wengine akiwemo rafiki yake (MM) tarehe 13/8/2006
wakiungana na wajumbe wengine wa mkutano mkuu kwa pamoja walisema
"...Sisi wajumbe wa mkutano mkuu tumeamua kuifanyia mabadiliko katiba ya
2004 ya chama chetu cha siasa kinachoitwa CHADEMA ili kuipa sura
inayoendana na mtazamo na msukumo mpya wa falsafa yetu ya nguvu na
mamlaka ya umma na dira na dhamira ya chama kuanzia 2006 na kuendelea.
Kuanzia sasa CHADEMA kitaendeshwa kwa mujibu wa katiba hii sambamba na
kanuni, taratibu na maadili ya chama...". Mwigamba na Zitto walitamka
kwa pamoja maneno hayo wakiwa na wajumbe wengine wa mkutano huo.
Msijiulize
kwa nini kwenye hili nawaongelea wote wakati aliyepeleka malalamiko kwa
msajili alikuwa Mwigamba peke yake! ukweli ni kwamba utatu huu wa
kisaliti nauongelea pamoja kwenye sakata hili kwa kuwa nyendo zote chafu
za kisaliti kwa sasa huwezi kuwatenga! Wanaruka pamoja, wanakutana na
kupanga pamoja na mawasiliano yao makubwa pamoja na mataniboi wao wa
kisiasa ni kuidhoofisha CHADEMA kuliko kuimarisha chama chao kinacho
undwa na viongozi walio saliti CHADEMA. Uhakika nilio kuwa nao,
watashindwa kama walivyo shindwa kupitia walicho kiita "Mkakati wa
mabadiliko 2013".
Mwigamba
kupitia gazeti la Mtanzania la tarehe 2/7/2014 alinukuliwa akimshukuru
Mungu kwa ofisi ya msajili kwa alicho kiita "..kusimamia na kueleza
ukweli wanachama wa CHADEMA kuhusu kuondolewa kinyemela kwa kipengele
cha ukomo wa madaraka.." akanukuliwa zaidi akisema "...CHADEMA
walinifukuza uwanachama wakiamini kuwa hoja ya kuvunja katiba niliyo
iwasilisha kwa msajili itatupwa na hatimaye amejiridhisha kuwa walikuwa
wamevunja katiba ya chama chao..."
Maelezo
ya Mwigamba yamejaa unafiki na hadaa zilizotawaliwa na dhambi ya
usaliti! Usaliti wa kukisaliti CHADEMA na sasa anajisaliti na yeye
mwenyewe! Hebu msome katikati ya mstari hapa "...hatimaye msajili
amejiridhisha kuwa walikuwa wamevunja katiba ya chama chao..." utadhani
marekebisho hayo yamefanyika yeye akiwa tayari kashasaliti na kwenda
ACT!
Kuna haja watu wajue, huyu Mwigamba alikuwa nani ndani ya
CHADEMA kabla ya kufukuzwa chamani kwa dhambi ya usaliti kupitia mkakati
wa mabadiliko na unafiki wa kumsifu mwenyekiti Mbowe kwa kuendesha
chama kwa ufanisi na ubunifu kwenye mkutano wa kanda ya kaskazini pale
Corridor Spring (Arusha) Novemba 2013 akiwa anawasilisha ripoti ya mkoa
wake (Arusha) huku robo saa baadae akimkashifu na kumtukana Mh Mbowe
kupitia akaunti yake bandia ya 'Mkulima maskini' kwenye mtandao wa
jamiiforums.
Mwigamba alikuwa nani kabla ya kusaliti CHADEMA?
1.
Mwigamba aliwahi kuwa mwanachama na kiongozi wa CHADEMA mkoa wa Arusha
mpaka alipo vuliwa nafasi zake zote za uongozi Novemba 2013.
2.
Aliwahi kuwa mhasibu wa chama makao makuu kuanzia 2011 hadi 2012 alipo
simamishwa kazi na makao makuu kutokana na matatizo mbalimbali moja
kubwa likiwa kushindwa kuleta ripoti ya matumizi ya fedha alizopewa
wakati wa uchaguzi mdogo wa Igunga ambapo zaidi ya milioni 210
zilitumika.
3. Alishiriki kwenye mkutano mkuu wa tarehe
13/08/2006 uliopitisha mabadiliko ya katiba toleo la mwaka 2006 akiwa
mjumbe kutoka mkoa wa Arusha (kwa mujibu wa kumbukumbu za mahudhurio).
4.
Amekuwa mjumbe wa vikao vya baraza kuu la chama toka 2009 alipo
chaguliwa kuwa mwenyekiti wa mkoa wa Arusha na amekuwa akishiriki vikao
mpaka Nov 2013 alipo vuliwa nyadhifa zote ndani ya chama.
5.
Amekuwa mjumbe wa vikao vya mkutano mkuu wa chama toka 2006 na amekuwa
akishiriki kwenye mikutano mikuu mpaka Novemba 2013 alipo vuliwa
nyadhifa zote ndani ya chama.
Lakini kubwa la muhimu ni kwamba, yeye
na Kitila Mkumbo ndio walikuwa wanamtandao wakubwa na waandaji wa
mkakati wa mabadiliko 2013 kinyume na maadili, itifaki, miongozo na
katiba ya chama kwa ajili ya rafiki wao anaye kamilisha UTATU wao wa
wasaliti. Lakini pia hawaja wahi kulalamika kwenye kikao chochote
kuhusiana na kipengele cha ukomo wa ungozi ndani ya kikao chochote cha
kikatiba.
Usaliti na hadaa za Samson Mwigamba na utatu wao wa kisaliti ni upi?!Pamoja na kujua kuwa alishiriki mchakato mzima wa mabadiliko ya katiba ya chama yeye na rafiki yake anajua kuwa:
1.0
wapo viongozi ndani ya CHADEMA ambao waliweza kuwa na haki ya kugombea
na walichaguliwa upya kwa zaidi ya vipindi viwili na hakuja wahi kuwa na
mgogoro kwani katiba ya chama ilifuatwa kwa ukamilifu wake.
Viongozi hao ni nani na wanatokea mikoa na kanda ipi?1.1.
Alhaji Ramadhani Kasisiko - mwenyekiti wa mkoa wa Kigoma na rafiki
mkubwa wa Zito Kabwe. (Inasemekana hata Hijjah alimpeleka yeye).
1.2.
Kansa Mbarouk - mwenyekiti wa mkoa Tabora, huyu ni ndugu na Athuman
Balozi (Tabora) aliyesoma tamko fake la waliojiita wajumbe wa baraza kuu
na mkutano mkuu pale Lamada Hotel na baadae wakaandamana kwenda kwa
msajili na CAG.
1.3. Msafiri Wamalwa - Katibu mkoa wa Kigoma.
Viongozi
hawa wote watatu hapo juu wanatokea kanda ya Magharibi (Tabora, Kigoma
na Katavi) ambako pia ni kanda aliyokuwa anatoka MM na Mzee Said Arfi.
Kwa
maana hiyo, kama Mwigamba angekuwa na dhamira safi angemuuliza rafiki
yake wa makakati wa mabadiliko aliyempa jina la MM au ange muuliza mzee
Said Arfi uhalali wa viongozi hao ambao walichaguliwa zadi ya vipindi
viwili.
2.0. Kama dhamira ya Mwigamba ingekuwa haiteswi na dhambi ya usaliti angejiuliza uhalali wa viongozi wengine ambao ni
2.1. Aliyekuwa mwenyekiti wa mkoa wa Singida na rafiki wa MM ambaye anaitwa
Nobert
Kitundu japo alikuja kujiuzuru kutoka na sakata la MM (huyu baadae
aliomba kurudi kuwa mwanachama wa kawaida baada ya kukiri kuwa alipewa
hela ili ajiuzuru kwenye ule upepo wa kujiuzuru ambao baadae ulikwama).
2.2.
Mwingine ni Mzee Stephen Massawe wa mkoa wa Dodoma ambaye mpaka sasa ni
katibu wa mkoa wa Dodoma na alipasifa za kugombea tena baada ya
mabadiliko ya katiba 2006 ambayo Mwigamba naye alishiriki mchakato wa
mabadiliko yake.
Viongozi wote hapo juu wanatokea kanda ya
kati yenye mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida, kanda ambayo anatokea
Dr Kitila Mkumbo ambaye ni rafiki mkubwa wa Mwigamba waliye shirikiana
kuandaa mkakati wa mabadiliki 2013 na ndio wanaunda utatu wa kisaliti
wakishirikiana na MM.
Kama Mwigamba hakuwa na nia ovu, kilicho mzuia asimuulize rafiki yake kwenye utatu wa kisaliti (Dr Kitila) ni nini?!
Itoshe
kusema kuwa, pamoja na viongozi hao hapo juu lakini pia wapo viongozi
wengine kama marehemu Philiph Magadula Shilembi ambaye naye alishika
uongozi kwa kuchaguliwa zaidi ya vipindi viwili, kama mtakumbuka huyu
marehemu alisha wahi kuandikiwa makala nzuri sana na MM na Mwigamba mara
baada ya kifo chake. Yupo pia mzee Shilungushela kutoka Shinyanga
ambaye pia mwenyekiti taifa baraza la wazee ambaye naye alichaguliwa kwa
kipindi cha tatu, Shilembi na Shilungushela wanatokea kanda ya ziwa
Mashariki yenye mikoa ya Shinyanga, Simiyu, na Mara.
Viongozi
wengine walio chaguliwa kwa vipindi zaidi ya viwili ni pamoja na mzee
Ndesamburo mwenyekiti wa mkoa wa Kilimanjaro na Mh Conchester Rwamlaza
(MB) ambaye ni katibu wa mkoa wa Kagera.
Nabaki najiuliza?!
1.
Kwa nini Mwigamba na utatu wake mtakatifu pamoja na mataniboi wao wa
kisiasa hoja yao iwe kwa viongozi wa chama taifa wakati kipengele cha
ukomo wa madaraka kama kingekuwepo kingehusu viongozi wote mpaka kwenye
ngazi ya misingi, matawi, kata, wilaya na hata mikoa na si mwenyekiti na
katibu mkuu taifa pekee?!
2.
Kwa nini Dr Slaa ahusishwe na kushambuliwa wakati nafasi yake ya
ukatibu mkuu na manaibu wake ni nafasi ya uteuzi na si nafasi ya
kugombewa na kupigiwa kura?! Nini kimejificha kumuongelea Dr Slaa na
wakati huohuo kumuongelea Mh Mbowe wakati mmoja anapigiwa kura na
mwingine anateuliwa?! Kumbuka hata rafiki wa Mwigamba kwenye utatu wa
usaliti (MM) hakuchaguliwa bali aliteuliwa na mwenyekiti kwenye miongoni
mwa majina yaliyo wasilishwa kwake kwa uteuzi na hivyo akawa naibu
katibu mkuu bara.
3.
Kwa nini rafiki na collegemates wa MM pale udsm ambaye naye ni rafiki
na Sisty Nyahoza ambaye ni mhudumu wa ofisi ya msajili waongee lugha
moja na kundi lote la utatu wa usaliti kuhusu kipengele cha ukomo wa
uongozi?! Lugha moja wanayoongea nikwa bahati mbaya au kuna ka mpango
nyuma ya pazia kampango ambako msajili wa vyama jaji Mutungi amejikuta
anaingizwa king na ameshtuka akiwa kwenye kilinge cha tope?!
4.
Mbona utatu wa usaliti hauongelei mabadiliko ya bendera ya chama pamoja
na mabadiliko makubwa yaliyo huisha mfumo wa chama kizima na wamejikita
kwenye kipengele kimoja tu ambacho bado ni halali kama vipengele
vingine wasivyo taka kuviongelea vilivyo halali?! Nashangaa kwa nini
hawaongelei mabadiliko ya bendera, organisation ya chama pamoja na
Redbrigade iliyopigiwa kelele na CCM ambayo haikuwemo kwenye katiba ya
2004?!
5.
Kama wameamua kusaliti uwepo wao na ushiriki wao kwenye mabadiliko ya
chama wakiwa na akili timamu, nani anaweza kusema kuwa watu hawahawa
kuwaita kuwa ni wenye kuungana na kuunda utatu wa usaliti na kuanzisha
chama chenye kuundwa na viongozi walio saliti CHADEMA hawapaswi kuitwa
kwa jina lingine kuwa wao ni Alliance for Cowards and Traitors yaani kwa
kifupi ACT?!
IMEANDIKWA NA: MOHAMED MTOI
Tuesday, 8 July 2014
HOME »
» UNAFIKI na USALITI wa Mwigamba dhidi ya tuhuma za ukomo madaraka katiba ya CHADEMA.
0 comments:
Post a Comment