HOME »
» PIGO JINGINE KWA, TAIFA STARS JONAS MKUDE NA HIMID MAO NAO MAJERUHI
VIUNGO
wawili wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Jonas Gerard
Mkude wa Simba SC na Himid Mao Mkami wa Azam FC ni majeruhi.
Kocha
Mkuu wa Stars, Mholanzi Mart Nooij amesema wachezaji hao wamerejea
kutoka Botswana ambako timu hiyo iliweka kambi ya wiki mbili wakiwa
majeruhi.
Maana
yake, nyota hao wako shakani kuichezea Stars katika mchezo wa mwisho wa
mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya Fainali za
Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Morocco dhidi ya Msumbiji Julai
20 mwaka huu.
 |
Himid Mao kushoto ni majeruhi |
Pamoja
na hayo, Nooij amesema kambi ya Botswana iliyodumu kwa wiki mbili
ilikuwa nzuri na imesaidia kuwajenga wachezaji wake baada ya kufanya
mazoezi na kupata mechi tatu za kujipima nguvu.
Stars
ilifungwa mechi mbili, moja dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo,
Botswana mabao 4-2 na nyingine dhidi ya timu ya jeshi la nchini humo,
BDF walishinda moja 3-1 na kufungwa moja 2-1.
Nooij
amesema wachezaji hao wapo katika kufanyiwa vipimo mjini Dar es Salaam
na baada ya hapo atajua uzito wa matatizo yao na pia kujua hatima yao
kuelekea mchezo na Msumbiji.
Tayari
Stars inamkosa kiungo mwingine, Frank Domayo wa Azam FC aliyefanyiwa
upasuaji wa nyama za paja nchini Afrika Kusini ambaye anatakiwa kuwa nje
ya Uwanja hadi mwakani.
0 comments:
Post a Comment