KLABU ya Arsenal imekubali kutoa Pauni Milioni 34 kwa Barcelona ili kumnunua mshambuliaji wa kimataifa wa Chile, Alexis Sanchez ingawa Barca wanasubiri kuona kama Juventus nap watatoa kiwango kama hicho.
Sanchez ameonyesha hataki kuhamia Liverpool licha ya jitihada zao za kumshawishi aende kuungana na kikosi cha Brendan Rodgers.
Hiyo inatokana na kwamba Liverpool nato imekubali kumuuza mshambuliaji wake, Luis Suarez kwa Barcelona.
Manchester City pia wanamtaka mchezaji huyo na wake tayari kumrudisha Hispania mshambuliaji wao Alvaro Negredo.
Liverpool
pia imetoa ofa ya Pauni Milioni 19.8 kwa ajili ya winga wa Benfica,
Lazar Markovic na mazungumzo yanaendelea kwa ajili ya mshambuliaji wa
Lille, Divock Origi kupitia wawakilishi wake nchini Brazil.
Juventus
iko vibaya kiuchumi na inakabiliwa na mtihani wa kumzuia mshambuliaji
wake Paul Pogba anayetakiwa na PSG na Manchester City.
Ataondoka? Juventus inaweza kumuuza Paul Pogba kuongeza fedha za kufika dau la Sanchez
0 comments:
Post a Comment