Sunday, 13 July 2014

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUFATA WELEDI NA KAZI ZAO

SAM_6582Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa akizungumza na waandishi wa habari katika kikao kilichofanyika katika ofisi za mbunge huyo. SAM_6590 
Baadhi ya waandishi wa habari wakichukua matukio
Na Denis Mlowe,Iringa
WANAHABARI mkoani Iringa wametakiwa kufata weledi wa kazi zao kwa kuelimisha jamii kwa kufanya kazi kulingana na maadili yao ya kazi na sio kwa maslahi ya vyama au mtu binafsi. Hayo yamesemwa na mbunge wa Iringa Mjini Mch Peter Msigwa wakati akizungumza na wandishi wa habari ofisini kwake juzi kuwa wanahabari wengi wamekuwa wakiandika habari ambazo zimekuwa hazina maadili kwa hofu ya baadhi ya vyama au viongozi fulani kuwatisha.
Msigwa alisema kuwa baadhi ya wandishi wa habari wamekuwa wakizuiwa kuzungumza na mbunge wa Iringa mjini kutokana na kuwa yupo katika chama cha upinzani.
Hata hivyo msigwa alisema kuwa wandishi wanatakiwa kuondokana na dhana hiyo na kutokuogopa kauli wanazotishiwa kwa kutokufanya kazi na mtu au chama fulani kutokana na kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria.
Aidha ameongeza kwa kusema kuwa wandishi wanapaswa kuandika habari zilizo na ukweli lakini pia panapopaswa kukosolewa wasisite kukosoa hata kama anayekosolewa akiwa ni kiongozi wa aina gani.
Msigwa alisema kuwa kiongozi yoyote anayezuia watendaji wake  kufanya kazi za jamii  hajui utendaji wa kazi zake. Aidha msigwa ameongeza kuwa viongozi wengi  wanashindwa kujua wajibu wao katika  ngazi walizopo akiwemo katibu mkuu wa  ccm mkoa wa Iringa kuingilia kazi za madiwani.

Related Posts:

0 comments: