Mbunge wa jimbo la Kilolo Prof. Peter Msola akimkabidhi mpira nahodha wa timu ya kijiji cha Mwatasi Inocent Myava.
Mbunge
wa jimbo la Kilolo Prof. Peter Msola akimkabidhi mpira nahodha wa timu
ya kijiji cha Mwatasi kwa upande wa wanawake Angelina Ngusa.
Na Denis Mlowe,Kilolo
VIJIJI 6 vya jimbo la Kilolo
katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa vimepata msaada wa mipira mitatu
kila kimoja kwa wanaume na wanawake pamoja shule moja kwa kila kijiji
kwa ajili ya kujiandaa na michezo mbalimbali inayotarajia kufanyika
wilayni humo.
Vijiji vilivyofaidika na msaada
huo ni kijiji cha Mwatasi, Mwangama, shule ya msingi Ng’ingula shule ya
msingi Bomalang’ombe, Masisiwe, Nyawegeti na Isanga ikiwa na thamani ya
sh. Laki tisa na nusu(9.5) zote za wilaya ya Kilolo.
Msaada huo ulitolewa juzi na
mbunge wa jimbo la Kilolo,Prof. Peter Msola wakati akizungumza na
wananchi wa kata Bomalang’ombe ikiwa ni utaratibu wake kuwatembelea
wananchi na kusikiliza kero zao kwa lengo la kukuza soka na mchezo wa
mpira wa mikono katika wilaya hiyo.
Akikabidhi msaada huo,Msola
alisema michezo ina nafasi kubwa ya kuajiri vijana na ni jukumu la wadau
kusaidia kukuza michezo yote na moja ya ahadi zake za kukuza michezo
katika wilaya ya Kilolo wakati akitaka ridhaa ya wananchi wa jimbo hilo
kuwakilisha kuwa mbunge wao.
Msola aliwaomba wananchi wa jimbo
hilo kuwekeza katika michezo kutokana kwa sasa imekuwa ajira ambayo
inawapatia kwa kiasi kikubwa maisha vijana na wale wote wanaoshiriki
michezo kama ajira.
Aidha Pro. Msola aliwaahidi
wanakazi wa kijiji cha Ng’ingula kuwapatia seti ya jezi mara baada ya
nahodha wa timu ya kijiji hicho kumtaka mbunge huyo kuwapatia msaada wa
jezi kutokana na kutokuwa nazo pindi ligi mbalimbali zinazoendeshwa
jiimboni humo ikiwemo mashindano ya kombe la jimbo ambapo yanadhaminiwa
na mbunge huo.
0 comments:
Post a Comment