MSHAHARA
wa Ashley Cole umepungua kwa Pauni 160,000 kwa wiki baada ya kutua AS
Roma ya Itali, kutoka Pauni 200,000 alizokuwa akilipwa Chelsea.
Cole alitua Italia jana na kusaini Mkataba wa miaka miwili kujiunga na timu hiyo ya Serie A kwa mshahara wa Pauni Milioni 1.8 kwa msimu (kiasi cha Pauni 35,000 kwa wiki).
Lakini mshahara wa mchezaji huyo unaweza kuongezeka hadi Pauni 80,000 kwa wiki kutokana na posho mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment