
Juu ya Baiskeli! Wachezaji wa England baada ya kipigo kutoka kwa Italia wamerudi Rio de
Janeiro kwenye kambi yao na kuanza kuipashia Uruguay.
ENGLAND wenye machungu ya kufungwa na
Italia mabao 2-1 katika mchezo wa ufunguzi wa kombe la dunia wameanza
maandalizi ya mchezo dhidi ya Uruguay.
Baada
ya kurejea Rio de Janeiro kambini kwao wakitokea Manaus, vijana wa Roy
Hodgson walitumia vikanyagio vya baiskeli kuongeza nguvu miguuni.
Wachezaji
walikuwa kwenye morali kubwa wakati wa mazoezi yao ndani ya Gym kwenye
Hoteli ya Royal Tulip na kusahau maamuzi ya jana usiku.

Nini kilitokea? Phil Jagielka, Joe Hart na Leighton Baines wakibadilishana mawazo wakati wakipasha moto misuli ndani ya gmy.
Kocha wa viungo Chris Neville akiongea na Glen Johnson wakati wa mazoezi.

Kata kiu mkaka!: Danny Welbeck akipiga fundo la kinywaji baada ya mazoezi.
0 comments:
Post a Comment