FOWADI WA COSTA RICA JOEL CAMPBELL
Campbell hajawahi kuichezea Arsenal na
kwa Misimu Mitatu sasa amekuwa nje kwa Mkopo tangu anunuliwe Agosti 2011
toka Klabu ya Saprissa.
Tangu wakati huo, Campbell amecheza kwa
Mkopo kwenye Klabu za Lorient, Real Betis na Msimu uliokwisha Mwezi Mei
alikuwa huko Ugiriki na Olympiakos.
Campbell, mwenye Miaka 21, Juzi alifunga
Bao wakati Costa Rica ikiwagaragaza Uruguay kwa Bao 3-1 kwenye Mechi
yao ya Kwanza ya Kundi D la Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil.
Akiongea na Wanahabari, Kijana huyo
alithibitisha: “Inabidi nirudi Arsenal, kwa sababu nina Mkataba nao.
Lakini kwa sasa kitu muhimu ni Nchi yangu na Kombe la Dunia!”
Mechi inayofuata kwa Costa Rica ni dhidi ya Italy na mwisho watamaliza na England kwenye Kundi D.
Campbell amesema: “Haikutushangaza kuifunga Uruguay, tumekuja hapa kushinda. Ndio maana unacheza Kombe la Dunia!”
THOMAS VERMAELEN KUTUA MANCHESTER UNITED?
Nazo habari kutoka Uingereza zinadai kuwa Nahodha wa Arsenal Thomas Vermaelen
huenda akahamia Manchester United.
Imeripotiwa kuwa Vermaelen tayari
ameshafikia makubaliano na Man United baada ya kupewa Nyongeza ya
Mshahara ya Pauni 30,000 na kumfanya awe juu ya Pauni Laki 1 kwa Mwezi.
Inasadikiwa Arsene Wenger hana
kipingamizi kwa Beki huyo kutoka Belgium kuhamia Old Trafford kwa vile
Meneja huyo wa Arsenal chaguo lake la Masentahafu ni Laurent Koscielny
na Per Mertesacker.
Inaaminika Arsenal watamuuza Vermaelen
kwa vile amebakiza Mwaka mmoja kwenye Mkataba wake ikiwa Man United
watalifikia Dau la Pauni Milioni 10 ambalo walimnunua kutoka Ajax Miaka
mitano iliyopita.
Mweyewe Vermaelen anapenda kujiunga na
Old Trafford ili aungane tena na Louis van Gaal, Meneja mpya wa Man
United, ambae walikutana huko Ajax.
\
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
KOCHA Arsene Wenger yuko tayari kumpa fursa Joel Campbell ya kuichezea Asernal. Kocha huyo wa Asernal ambaye yupo mjini Porto Alegre kama mtangazaji wa Televisheni ya Ufaransa, jumapili jioni alishuhudia Ufaransa ikichapa Honduras maao 3-0.
Lakini Wenger amethibitisha kuwa amepanga kumrudisha tena katika kikosi cha Asernal nyota huyo wa Cost Rica ambaye alifanya kazi nzuri wakiizamisha Uruguay. Kocha huyo mnamo mwaka 2011 alimtoa kwa mkopo nyota huyo mwenye miaka 21.
\
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Joel Campbell aliisaidia Costa Rica kuibamiza Uruguay siku ya jumamosi.
KOCHA Arsene Wenger yuko tayari kumpa fursa Joel Campbell ya kuichezea Asernal. Kocha huyo wa Asernal ambaye yupo mjini Porto Alegre kama mtangazaji wa Televisheni ya Ufaransa, jumapili jioni alishuhudia Ufaransa ikichapa Honduras maao 3-0.
Lakini Wenger amethibitisha kuwa amepanga kumrudisha tena katika kikosi cha Asernal nyota huyo wa Cost Rica ambaye alifanya kazi nzuri wakiizamisha Uruguay. Kocha huyo mnamo mwaka 2011 alimtoa kwa mkopo nyota huyo mwenye miaka 21.
‘Hakika atarudi kwetu wakati wa maandalizi ya msimu," Wenger aliwaambia Sportsmail. "Ameimarika vizuri".
Wenger iliikosa mechi ya Costa Rica
kwasababu alisafiri kwenda Porto Alegre, lakini alipokea ujumbe kutoka
kwa kocha wa zamani wa Chelsea Avram
Grant, ambye yuko na luninga ya Israel akimtaarifu jinsi ambavyo
Campbell alicheza vizuri.
Campbell aliifungia Costa Rica bao moja na kutengeneza nafsi moja katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Uruguay mjin Fortaleza.
Campbell
alisaini mkataba na Asernal miaka mitatu iliyopita, lakini muda mrefu
amecheza kwa mkopo , lakini Wenger anahisi sasa imefika muda muafaka wa
kumrudisha katika timu ya kwanza ya klabu yake.
Mara ya kwanza alipelekwa kwa mkopo
katika klabu ya Lorient nchini Ufaransa, halafu Real Betis nchini
Hispania na kwasasa anaichezea timu ya Ugiriki ya Olympiacos, ambapo
amewavutia Manchester United
katika michuano ya ligi ya mabingwa.
0 comments:
Post a Comment