SOMA ZAIDI:
Release No. 106
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Juni 16, 2014
RAMBIRAMBI MSIBA WA GEORGE MPONDELA
Kwa mujibu wa klabu ya Yanga, Marehemu
Mpondela anatarajiwa kuzikwa Alhamisi (Juni 19 mwaka huu) jijini Dar es
Salaam, na msiba upo Kigamboni Mnarani.
Mpondela alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu
wa klabu ya Yanga katika uchaguzi uliofanyika mwaka 1994 baada ya
kumshinda aliyekuwa mpinzani wake wa karibu George Ndaombwa.
Msiba huo ni mkubwa katika familia ya
mpira wa miguu nchini kwani, Mpondela enzi za uhai wake alitoa mchango
mkubwa akiwa kiongozi katika klabu yake ya Yanga.
TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu
Mpondela, na klabu ya Yanga na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu
katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Taratibu zaidi za mazishi zitatolewa na
Yanga baada ya kufanya mawasiliano na familia ya marehemu Mpondela.
Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Amina.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 comments:
Post a Comment