Wednesday, 9 July 2014

MARADONA: KUFUZU FAINALI TUNAMTEGEMEA LIONEL MESSI KWA KILA KITU

Maradona: World Cup fate depends on Messi
 

GWIJI wa Argentina, Diego Maradona anaamini ndoto za taifa lake kutinga fainali ya kombe la dunia dhidi ya Uholanzi leo hii zimebebwa mabegani kwa Lionel Messi.
 Maradona amesema wanashukuru kwasababu wana mshambuliaji wa Barcelona ambaye amewapa mafanikio katika mashindano ya mwaka huu.
 Messi amefunga mabao manne katika mechi tano alizocheza katika mashindano ya mwaka huu na bado ana presha ya kufanya vizuri leo kutokana na majeraha aliyonayo Angel Di Maria, ila Maradona anajiamini kuwa nyota huyo atafanya vizuri.
 “Ni kwasababu ya Messi ndio maana tumefika hatua ya nne bora kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1990 na bao moja tu litatufanya tufike karibu na malengo yetu. Lakini haitakuwa rahisi”. Maradona amewaambia Times of India.
 “Kila kitu tunategemea kwa Messsi ambaye atabaki kuwa mchezaji bora bila kujali matokeo yatayopatikana”.
 “Hakuna mchezaji bora kama Messi. Kwasababu hachezi soka la nyumbani, wengi wanamtazama kwa kupitai TV”.
 “Baada ya kushindwa kufika robo fainali mwaka 2006 na 2010 na yeye akiwa sehemu ya kikosi, mwaka huu umeongeza matarajio”.
 Kwa mara ya mwisho, Argentina alishinda kombe la dunia 1986 walipoifunga Ujerumani Magharibi mabao 3-2 kwenye mechi ya fainali.

Related Posts:

0 comments: