Kiingilio
cha chini cha mechi kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Msumbiji (Mambas)
itakayochezwa Julai 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
kitakuwa sh. 7,000.
Tiketi
zinapatikana kwa mfumo wa elektroniki kupitia M-PESA. Kiingilio hicho
kwa ajili ya viti vya rangi ya rangi ya chungwa, kijani na bluu.
Viingilio katika maeneo mengine vitatangazwa baadaye.
Mshabiki
ili apate tiketi anatakiwa kutumia M-PESA kwa kupiga *150*00# kisha
bonyeza 4, ingiza namba ya kampuni 173399 kisha weka 7000 kwenye namba
ya kumbukumbu ya malipo, na weka 7000 kama kiasi cha bei ya tiketi na
mwisho weka namba yao ya siri.
Baada
ya hapo utapokea ujumbe wenye orodha ya vituo vya MaxMalipo kwa ajili
ya kuchukulia tiketi ukiwa na namba ya uhakiki wa malipo yako.
Vituo
vya kuchukulia tiketi ni mgahawa wa Steers uliopo mtaa wa Samora/Ohio,
maduka makubwa ya Uchumi Supermarket (Quality Centre, Tabata Segerea na
kituo cha daladala Makumbusho), Sheer Illutions (Millennium Tower na
Mlimani City), maduka makubwa ya TSN Supermarket (City Centre, Kibo
Tegeta na Upanga).
Vodashop
(Ubungo na Mill Pamba), Shop Mwenge (Born to Shine), Puma Petrol
Station (Mwenge na Uwanja wa Ndege), Engen Petrol Station (Mbezi Beach),
Big Bon Petrol Station (Kariakoo, Sinza Mori, Mbagala na Temeke), YMCA
(Posta Mpya), City Sports Lounge (Posta), Uwanja wa Taifa) na ofisi za
TFF (PPF Tower).
Na Boniface Wambura, Dar es salaam
0 comments:
Post a Comment