Makamu mwenyekiti Uenezi CHADEMA kanda ya Magharibi Deogratius Liyunga akiwa amelazwa katika Hospital ya Maweni)baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana(Picha na Editha Karlo)
Na Editha Karlo,Kigoma
WATU
wasiojulikana wamemvamia na kumpiga pamoja na kumjeruhi sehemu
mbalimbali za mwili kwa kutumia vitu vyenye ncha kali Makamu Mwenyekiti
wa uenezi kanda ya Magaharibi Deogratius Liyunga na kupelekea kulazwa
katika Hospita ya Mkoa wa Kigoma(Maweni).
Tukio
hilo limetokea jana majira ya saa tano usiku katika eneo la Mlole
Manispaa ya Kigoma Ujiji,wakati kiongozi huyo akiwa njiani kurudi
nyumbani kwake akitokea eneo la Mwanga kuangalia mechi za kombe la
Dunia.
Akiongea
na mtandao huu wodini nalipolazwa juu ya tukio hilo kiongozi huyo
alisema kuwa alibakiza hatua 25 iliaweze kuingia nyumbani kwake ghafla
walitokea wanne,mmoja alimvamia na kumkaba shingo huku wale wengine
wakimshambulia kwa kisu,nyembe na ubao.
Alisema
mbali ya watu hao kumpiga na kumjeruhi lakini walimpora fedha kiasi cha
shilingi 63,000 ingawa hawakufanikiwa kumpora simu yake ya mkononi
iliyokuwa mfukoni.
Baada
ya watu hao waliomvamia kuondoka alifanya mawasiliano kwa watu wake wa
karibu wakiwemo wanachama wa CHADEMA ambao walifika eneo la tukio na
kumkimbiza Hospital kwaajili ya matibabu.
Makamu Mwenyekiti alisema
kuwa tukio hilo lililomkuta linahusiano mkubwa na masuala ya kisiasa
kwani kabla ya tukio hilo amekuwa akipokea ujumbe wa fupi wa maneno ya
vitisho kwenye simu yake ya mkononi kutoka kwa watu wanaodaiwa kuwa ni
wananchama wa chama kipya cha ACT.
”Mimi hiyo taarifa sijaipata ofisini kwangu bado ndo nina isikia kutoka kwako ngoja nifuatilie nitakujulisha”alisema Kashai
0 comments:
Post a Comment