KOCHA wa Sao Paulo inayocheza ligi
kuu ya Brazil, Muricy Ramalho amesema Pep Guardiola na Jose Mourinho wanafaa
kuwa warithi wa Luiz Felipe Scolari katika nafasi ya ukocha mkuu wa timu ya
taifa ya Brazil.
Hatima ya kocha wa sasa wa Brazil
imekuwa matatani kufuatia The Selecao kupigwa kipondo cha aibu cha mabao 7-1
dhidi ya Ujerumani katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la dunia iliyofanyika
Belo Horinzonte jumanne ya wiki hii.
Kuelekea katika mchezo wa mshindi wa
tatu baina ya Brazil dhidi ya Uholanzi usiku wa leo, Ramalho, ambaye pia
anatajwa na Zico kurithi mikoba ya Scolari, ametaja majina maarufu ambayo
anaamini yanaifaa kazi hiyo.
“Mpira uko hapa mpaka sasa, “ kocha
huyo mwenye miaka 58 amewaambia ESPN
Brasil.
“Wakati umefika na nadhani kocha wa
zamani wa Corinthians, Tite anastahili . Ameshinda makombe mengi. Lazima awe
katika orodha ya watakaotajwa”.
“Kama sio Mbarazil, itakuwa vizuri
zaidi. Guardiola atakuwa chaguo langu la kwanza. Au Mourinho. Tunatakiwa kuwa
na makocha wa kiwanggo cha juu, ambao wana soko hata kibiashara. Watendaji
wazuri wa kazi”.
“Kati ya hao wawili, naweza kusema
Guardiola. Lakini itakuwa juu ya CBF (shirikisho la soka la Brazil) kuamua.
Haya ni maoni yangu na nayaweka wazi”.
Ramalho alikuwa na nafasi ya kuwa
kocha wa Brazil mwaka 2010, lakini aliendelea kubaki Fluminense na anasema
hajutii kukosa nafasi hiyo na wala hana mpango wa kuomba.
“Mimi sina uchu wa madaraka”. Alisema.
0 comments:
Post a Comment