*Ni baada ya wataalam kukiuka maagizo yake aliyotoa Machi mwaka huu
ILE
HALI ya kufanya kazi kwa mazoea (business as usual) iliyojengeka kwa
baadhi ya watendaji wa Serikali leo imewatokea puani watendaji wa
Manispaa ya Dodoma wakati Waziri Mkuu alipoamua kufanya ziara kukagua
miradi ya maendeleo.
Akiwa
katika eneo la kwanza ambalo alipangiwa kukagua ujenzi wa kituo cha
afya cha Mkonze leo asubuhi (Jumamosi, Juni 7, 2014) Waziri Mkuu
alipokea taarifa ya ujenzi wa kituo na kubaini kuwa hawajafanya chochote
ili kutekeleza maagizo yake aliyoyatoa Machi 22, 2014.
Katika
taarifa yake, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Mhandisi Lusako
Kilembe alimweleza Waziri Mkuu kwamba walifanya tathmini ya ujenzi wa
kituo hicho na kubaini kuwa zinahitajika sh. Milioni 24.15 na kwamba
maombi ya matumizi hayo yamepangwa kujadiliwa kwenye kikao cha kamati ya
fedha na uongozi kitakachofanyika Juni 10, mwaka huu.
Akiwa
katika maadhimisho ya kilele cha wiki ya maji ambayo Kitaifa
yalifanyika mkoani Dodoma, Waziri Mkuu alizindua mradi wa maji jirani na
kituo cha afya cha Mkonze na kubaini kuwa kuna hitilafu za ujenzi.
Ndipo akaagiza kwamba ufanyike ukarabati na yeye akaahidi kuja kukagua
ukarabati huo mwezi Juni, 2014.
Mara
baada ya kusomewa taarifa ya mradi, Waziri Mkuu akahoji ni kwa nini
hawajafanya chochote tangu alipotoa maelekezo Machi, mwaka huu. Hakupata
jibu la kueleweka kutoka kwa viongozi wa wilaya na mkoa.
Waziri
Mkuu aliwasalimia wananchi waliokuwepo kwenye eneo hilo na kuwaeleza
kwamba hawezi kukagua kituo hicho ilhali hakuna kilichotekelezwa tangu
afike hapo Machi mwaka huu.
Alisema
haiwezekani yeye atoe maagizo katika kipindi chote hicho halafu
kisifanyike kitu chochote. Akaondoka na kuendelea na ziara hadi kijiji
cha Manzase ambako alikagua mradi wa kisima cha maji.
Mapema,
katika taarifa yake, Mhandisi Kilembe alisema kituo hicho cha afya
kilijengwa chini ya ufadhili wa ubalozi katika makubaliano yaliyofikiwa
Novemba 11, 2009 kwamba ingetoa dola za marekani 84,307 sawa na sh.
Milioni 152.86.
Hata
hivyo, mara baada ya ujenzi kukamilika Agosti 29, 2012, kituo hicho
kilipata nyufa nyingi hali iliyosababisha kifungwe na wananchi walitoa
malalamiko yao kwa Waziri Mkuu Machi mwaka huu wakati alipokwenda
kuzindua mradi wa maji kwenye kijiji cha Mkonze jirani na kituo hicho.
0 comments:
Post a Comment