KATIKA
hali isiyo ya kawaida mchekeshaji maarufu, Mujuni Sylivester 'Mpoki,'
ametangaza rasmi mgogoro na waandishi wa habari kwa kutoongea nao kwa
madai kwamba wengi wao hawana akili.
Bila ya
kutaja sababu ya kufikia uamuzi huo hata pale alipooulizwa na safu hii,
Mpoki alisema ameshajiapiza kutoongea nao, msimamo ambao anaamini
atausimamaia katika maisha yake.
Wakati
akiweka msimamo huo, tetesi zilizoifikia safu hii ni kwamba Mpoki
ametangaza mgomo huo baada ya kukosolewa na vyombo vya habari ikiwamo
mitandao ya kijamii, kwa kuwatusi wasanii mbalimbali na waalikwa wengine
wakati akiwa MC katika tukio la Tuzo za Muziki za Kilimanjaro'KTMA
2014' zilizofnyika usiku wa Mei 3 kwenye Ukumbi wa Mlimani City.
CHANZO TANZANIA DAIMA
CHANZO TANZANIA DAIMA
0 comments:
Post a Comment