Wednesday, 11 June 2014

WAMAJINGA WATAWANYWA KWA MABOM MKOANI MWANZA

 
JESHI la Polisi mkoani Mwanza, limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafanyabiashara ndogo (wamachinga) waliokuwa wanapinga kuondolewa katika eneo la Kempu na eneo la soko la Makoroboi jijini humo.
Aidha, hatua hiyo imesababisha vurugu na kusimamishwa kwa shughuli mbalimbali za kijamii, ikiwemo kufungwa kwa maduka hadi katikati ya eneo la jiji na baadhi ya huduma ya usafiri kukosekana kwa muda katika barabara zinazokatiza katikati ya jiji hilo, ambapo kuanzia saa nne asubuhi hadi tunaenda hewani mashuhuda wanasema vurugu hizo bado zinaendelea.
Vurugu-wamachinga-Mwanza
Vurugu-wamachinga-Mwanza
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Valentino Mlowola, ameuambia mtandao huuleo Juni 11, 2014 kuwa Jeshi hilo limelazimika kutumia mabomu hayo ili kuwatawanya wafanyabiashara hao waliokuwa wakihatarisha amani na kusema bado hakuna mtu yeyote aliyeripotiwa kujeruhiwa katika vurugu hizo.
Serikali yatakiwa kuingilia kati migogoro ya wamachinga
Akiomba mwongozo Bungeni mjini Dodoma, Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje, ameitaka serikali kusitisha zoezi hilo ili kutafuta njia mbadala ya kushughulikia migogoro kati ya serikali na wamachinga.
Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, amesema kuwa
 chanzo Fikra Pevu -   in  JamiiForums

Related Posts:

0 comments: