Mwezi Mei, Man City waliadhibiwa na UEFA
kwa kupigwa Faini na Kikosi chao cha Ulaya kupunguzwa kuwa Wachezaji 21
tu huku kati yao wakitakiwa 8 kuwa wale ‘Waliokuzwa Nyumbani’ baada ya
kuvunja Sheria za FFP zinazotaka Klabu kujiendesha kwa Faida kutokana na
Mapato yao wenyewe.
Hata hivyo, baada ya FIFPro, Chama cha
Kutetea Haki za Wachezaji wa Kulipwa, kuikabili FIFA na kuitaka
isiadhibu Wachezaji badala ya Klabu, UEFA imelegeza Adhabu.
Katibu Mkuu wa UEFA, Gianni Infantino,
amesema: "Hili limekuja baada ya ombi la FIFPro ambao walisema Adhabu
zinaadhibu Wachezaji wenye Mikataba badala ya Klabu!””
FFP-NI NINI?
-Ni Financial Fair Play
-UEFA ilianzisha Club Financial Control Body (CFCB) Juni 2012 ili kudhibiti Klabu kutotumia Fedha zaidi ya Mapato yao wenyewe.
- Kanuni za FFP zitaanza kikamilifu
Msimu ujao, 2014/15, ingawa Klabu zilitakiwa kuzifuata kwa Miaka miwili
sasa na ndio maana ManCity imekumbwa na Adhabu.
Infantino alisema kwa sababu hiyo ndio
maana wameamua kupunguza idadi ya Wachezaji ‘Waliokuzwa Nyumbani’ iwe na
uwiano sawa na Kikosi cha Man City kilichopunguzwa.
Mbali ya kupunguziwa Kikosi chao cha
Ulaya, City pia walidungwa Faini ya Pauni Milioni 49 huku Milioni 32
ikisimamishwa na pia kutakiwa kutumia Pauni Milioni 49 tu kununua
Wachezaji na hii ikijumuisha Fedha zozote watakazopata wakiiuza
Wachezaji.
Pia, Fungu la Mshahara wa Wachezaji wao limetakiwa libaki vile vile kama ilivyokuwa Msimu wa 2013/14.
Msimu wa 2013/14, City kwenye UEFA
CHAMPIONZ LIGI walisajili Wachezaji 23, 8 wakiwa Wachezaji ‘Waliokuzwa
Nyumbani’, na kuwatumia 21 kati ya hao.
Katika hao 8, Kipa Joe Hart, Jack Rodwell, lGael Clichy na Dedryck Boyata walikuwemo.
Tafsiri ya UEFA ya Wachezaji ‘Waliokuzwa
Nyumbani’ haijali Uraia ili mradi Mchezaji husika awe amefundishwa na
Klabu hiyo au nyingine, zote zikiwa chini ya Chama kimoja cha Mpira cha
Nchi hiyo, kwa muda usiopungua Miaka Mitatu wakati Mchezaji akiwa na
Umri kati ya Miaka 15 na 21.
0 comments:
Post a Comment