Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha
Magubike Bi Lenatha Mbilinyi kushoto akipokea msaada wa saruji mifuko
100 kutoka kwa mbunge wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa leo
,wanaoshuhudia kulia ni katibu menezi wa CCM wilaya Denis Lupala na
diwani wa kata ya Nzihi katikati Bw Stivin Mhapa
........................................................................................
MBUNGE wa jimbo la
Kalenga mkoani Iringa Godfrey Mgimwa
ameanza kutimiza ahadi zake kwa
wananchi wa jimbo la kalenga kwa
kukabidhi mifuko zaidi ya 150 ya
saruji katika kijiji cha Magubike
na kijiji cha Kidamali kata ya Nzihi
yenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 2.5
Saruji hiyo mifuko
100 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa
jengo la utawala shule ya sekondari
Dimitrios katika kijiji cha Magubike
na mifuko 50 kwa ajili ya shule ya sekondari Kidamali.
Mgimwa alisema kuwa lengo la kutimiza ahadi yake
hiyo ni kama njia ya
kuwashukuru wana Kalenga kwa
kumchagua katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni pia kutimiza ahadi
mbali mbali binafsi ambazo alizitoa mbunge aliyefariki marehemu Dr Wiliam
Mgimwa.
Alisema ataendelea
kutimiza ahadi binafsi
zilizotolewa na marehemu Dr Mgimwa kulingana na uwezo wake
na zile za kitaifa ambazo zipo katika Ilani ya CCM
atahakikisha anaikumbusha serikali ya CCM ili
kutimiza ahadi hizo kwa wakati.
“Ndugu zangu wananchi mbali
ya kuwa ubunge
wangu ni wa mwaka mmoja
ila tayari mimeanza
kutimiza ahadi bila ya kuchelewa
na ninawahakikishieni sita
waangusha nitaendelea kufanya
hivyo zaidi mniombee
uzima”
Alitaja maeneo ambayo tayari
amekabidhi ahadi zilizotolewa na mbunge aliyefariki kuwa ni pamoja na Kiwere shule ya msingi mifuko 80 ya
saruji,shule ya msingi wangama bati 100
na saruji mifuko 50,shule ya msingi
Negabii bati 100 ,shule ya msingi Mibikimitali bati 50 ,Kijiji cha Isupilo bati
50 na saruji mifuko 50 na maeneo mingine
mengi.
Pia amekabidhi kiasi cha
Tsh 500,oo kwa ajili ya kuchangia kuwezesha kusajili
timu ya kata ya Nzihi na
nyingine kwa ajili ya ukarabati wa soko
|
0 comments:
Post a Comment