Wakulima wa mazao mbalimbali mkoani Iringa wametakiwa kutumia mbegu za kisasa ili kuboresha shughuli za kilimo na kupata mazao ya kutosha.
Afisa miradi wa muungano wa wakulima vijijini Bw William Maja
aliyasema hayo akiwa na baadhi ya wakulima katika ukumbi wa shule ya msingi Chemi Chemi iliyopo katika manispaa ya Iringa ambapo aliwataka wakulima walime zao la mtama.
Hata hivyo alisema kuwa wakulima wanapaswa kushirikiana katika kilimo na kuacha dhana ya kutegemea watu wachache katika kilimo ili kufanikiwa zaidi.
Aidha alisema kuwa wakulima pindi wanapopanda mazao watumie mbolea husika ili waweze kupata mazao ya kutosha.
NA DIANA BISANGAO WA IRINGA
0 comments:
Post a Comment