Mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la Lameck Mashaka (38) mlinzi na mkazi wa
kijiji cha Mgowelo mkoani Iringa amefariki dunia baada ya kugongwa na
tela alilokuwa akililinda.
Akizungumza na mtandao huu wa ofisini
kwake Kamanda wa polisi mkoani hapa ACP Ramadhani Mungi alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 4 Juni majira ya saa
7:30 usiku huko maeneo ya Kware Ruaha Mbuyuni barabara kuu ya Iringa –
Moro iliyoko wilaya ya Kilolo.
Kamanda
Mungi alisema gari aina ya Scania yenye namba za usajili T. 903 ARK
iliyokuwa ikiendeshwa na Rajabu Aungalipa (36) mkazi wa Mbagara Dar es
salaam liliacha njia na kasha kuigonga Tela lenye namba T. 894 BDQ
iliyokuwa imeegeshwa kando ya barabara.
Alisema
mbali na mtu mmoja kufariki dunia pia ajali hiyo ilisababisha majeruhi
watatu ambao ni Ramadhani Dunia (23) ambaye ni fundi magari, Rajabu
Aungalipa (36) ambaye ni dereva wa scania pamoja na Farid Ruben ambao
wote wamelazwa katika hospitali ya Tandika iliyopo jijini Dar es Salaam.
CHANZO
www.matukiodaima.com
CHANZO
www.matukiodaima.com
NA DIANA BISANGAO WA IRINGA
0 comments:
Post a Comment