KOCHA wa Manchester United, Louis Van
Gaal amemuagiza mkurugenzi mkuu wa klabu hiyo, Ed Woodward, kumuuza
Marouane Fellaini kwa madai kuwa sio aina ya mchezaji anayetakiwa
kukipiga Old Trafford.
Fellaini ameonesha kiwango kizuri
katika fainali za kombe la dunia na kuibua maswali kama Van Gaal
ataendelea kumbakisha nyota huyo aliyesajiliwa na David Moyes kwa ada ya
uhamisho ya paundi milioni 27 kutoka Everton.
Lakini tayari Van Gaal ameshaagiza kuuzwa kwa mchezaji huyo kabla msimu mpya haujaanza.
MPENJA BLOG inafahamu Van Gaal amewaambia watu wanaohusika na Fellaini kuwa 'sio aina ya mchezaji wa Man United".
Vyanzo vya habari kutoka Old Trafford
wiki hii vimeeleza kuwa Van Gaal ameweka wazi nani anamtaka na nani
hamtaki katika kikosi chake na tayari amemwambia Ed Woodward.
Lakini inaonekana United haitaweza
kumuuza Fellaini kwa kiwango cha paundi milioni 27 kama wao
walivyomnunua kutoka Everton mwezi septemba mwaka jana.
Ameimarika: Mchezaji wa Ubelgiji, Marouane Fellaini angalau amefurahia kombe la dunia nchini Brazil.
Kocha aliyetimuliwa Man United, David
Moyes alimlinda Fellaini msimu ulipoita na alikuwa anasema nyota huyo
mwenye miaka 26 alikuwa na kiwango kizuri, lakini hakuizoea United.
Kwasasa kama Fellaini anataka
kuichezea United msimu ujao anatakiwa kuonesha kiwango cha juu katika
mechi zilizosalia za kombe la dunia.
Hana huruma akiwa kazini: Louis van Gaal ameweka wazi wachezaji wanaowataka mara atakapoanza kazi.
0 comments:
Post a Comment