Hana bei: Rais wa Barcelona amesema Lionel Messi hauziki.
RAIS wa Barcelona imesisitiza kuwa
Lionel Messi "hauziki" wakati huu miamba hiyo ya katalunya ikihangaika
kumuongeza katika kikosi chao Luis Suarez msimu ujao.
Kwa sasa Messi anaichezea timu ya taifa
ya Argentina katika fainali za kombe la dunia na ameshafunga mabao manne
na kuifikisha hatua ya robo fainali.
Nyota huyo mwenye miaka 27 siku za karibuni alisaini mkataba na Barcelona ambao utamuingizia paundi milioni 16.3 kwa mwaka.
Rais wa klabu, Josep Maria Bartomeu
alisema: "Nikiwa nahusika moja kwa moja, Messi hataki kuondoka. Tulimpa
mkataba mpya siku si nyingi na ana furaha".
Kiungo wa Barca , Xavi (kulia) bado hajaamua hatima yake
Bartomeu pia alisema Xavi anaweza kuondoka klabuni hapo, lakini hajaamua bado ataelekea wapi.
"Xavi ana haki ya kuamua anataka kufanya
nini na tutaheshimu suala hilo. Siku moja atarudi klabuni kwasababu ana
uwezo wa kuwa kocha mkubwa".
Barcelona walishafungua ofa ya paundi
milioni 72 siku ya jumatano usiku, lakini Liverpool wanata mkwanja wa
paundi milioni 80 ili kumuuza nyota huyo mwenye miaka 27.
Enlarge
Messi akitaniana na mchezaji mwenzake wa Argentina Fernando Gago.
0 comments:
Post a Comment