Washiriki
wa Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wakiwa jukwaani
wakati wakiigiza moja ya Igizo walilopewa na Mwalimu wao Dk Mona
Mwakalinga katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa siku ya Jumanne ya Wiki
inayomalizika leo.Igizo hilo ni la kwanza kwaajili ya mchujo kwa
washiriki
Vijana wakiendelea na Kazi Jukwaani
Vijana
wakiwajibika katika jukwaa kwaajili ya kuwania tiketi ya kuzisaka
Milioni 50 za kitanzania katika fainali itakayofanyika mwisho wa mwezi
wa nane.
Josephat Lukaza – Proin Promotions Limited – Dar Es Salaam.
Shindano
la Tanzania Movie Talents (TMT) limeingia hatua nyingine ambapo sasa
washiriki wa fainali ya Shindano hilo kuanza kupigiwa kura na
watazamaji. Washiriki hao 20 kutoka kanda sita za Tanzania wanaendelea
na kambi huku wakipewa mafunzo juu ya sanaa ya uigizaji na uandikaji wa
muswada (script) kutoka Kwa Mhadhiri wa Sanaa kutoka Chuo Kikuu Cha Dar
Es Salaam, Dk Mona Mwakalinga.
Washiriki
hao 20 sasa watapigiwa kura na watazamaji kutoka na kuonyesha uwezo wao
wa kuigiza na kuwavutia watazamaji kwa vipaji vyao. Kipindi cha Kwanza
cha Mchujo kimeonyeshwa hapo jana Kupitia kituo cha Runinga cha ITV
ambapo sasa watazamaji wameweza kujionea uwezo wa kila Mshiriki katika
Shindano hilo.
Vipindi
vya TMT vitaendelea kurushwa kupitia ITV kila Jumamosi saa NNE USIKU na
kurudiwa Jumapili Saa KUMI JIONI na JUMATANO SAA TANO USIKU, usikose
kutazama ni mshiriki yupi mwenye uwezo na aliyekuvutia ili uweze
kumpigia kumpigia kura
Jinsi
ya Kumpigia Kura Mshiriki umpendae unaenda upande wa Meseji kwenye Simu
yako na Kuandika “TMT” ikifuatiwa na Namba ya Mshiriki halafu unatuma
kwenda 15678. Mfano: TMT00 halafu unatuma kwenda 15678. Vigezo na
masharti kuzingatiwa.
Fainali
ya Shindano la Tanzania Movie Talents litafanyika Mwisho wa Mwezi wa
Nane ambapo mshindi mmoja atajinyakulia kitita cha Shilingi Milioni 50
za Kitanzania
0 comments:
Post a Comment