Tangazo rasmi: Arsenal walitangaza hadharani usajili huo kupitia mtandao wake wa Twita ambapo waliweka picha na ujumbe.
KLABU ya Arsenal imemsajili beki wa kulia wa Ufaransa Mathieu Debuchy kutokea klabu ya Newcastle.
Debuchy, mwenye miaka 28,
amesajiliwa kwa nia ya kuziba pengo la beki wa kulia, Mfaransa
mwenzake, Bacary Sagna aliyetimka Emirates na kujiunga na mabingwa wa
ligi kuu, Manchester City majira haya ya kiangazi mwaka huu.
Asernal alitweet picha ya Debuchy ikisindikizwa na ujumbe uliosomeka #Karibu Debuchy.
Jembe jipya: Debuchy aliichezea Ufaransa mechi nne kati ya tano za kombe la dunia nchini Brazil na alionesha kiwango cha juu.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment