Na Mahmoud Ahmad, Arusha
MUFTI Shekh Mkuu wa Tanzania, Issa Bin Shaaban Simba, jana ameondoa sitofahamu ya muda mrefu kuhusu uongozi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa, uliopo Bondeni Manispaa ya Arusha na Masjid Quba, kwa kuwataja viongozi wanaostahili kuwepo madarakani.Kabla ya kuwataja viongozi hao, alisema kuwa kwa muda mrefu kumekuwa na uongozi wa bakwata katika ngazi za juu za Mkoa, ambao umesababishwa na ukaidi wa makusudi wa baadhi ya watu kukiuka utaratibu wa katiba ya BAKWATA juu ya upatikanaji uongozi katika ngazi hizo.
Alisema hali hiyo imesababisha kuw ana makundi mawili ya uongozi katika ngazi ya Mkoa, Wilaya ya Arusha, Msikiti Mkuu wa Ijumaa Arusha Mjini na Masjid Quba, jambo linalokwamisha maendeleo ya Uislamu Mkoani Arusha.
Mufti Shekh Simba alisema kutokana na hali hiyo amelazimika kufanya ziara Mkoani Arusha na kukutana na viongozi wa serikali,viongozi wa BAKWATA wa makundi yote yanayokinzana.
Alifafanua upatikanaji wa viongozi katika ngazi Msikiti chini ya uongozi wa Mtaa, Wilaya, Mkoa na taifa kuwa ni lazima kufuata katiba ya Bakwata ya mwaka 199 toleo la mwaka 2008, Ibara ya 10 ya katiba inayozungumzia muundo wa Bakwata ili kutekeleza mipango na shughuli
zake.
Aidha alisema katika sheria hiyo inasema kuna aina mbili za uongozi katika ngazi zote, ambazo ni wale wa kuchaguliwa na kuteuliwa.
Alisema kutokana na utaratibu huo sheria hiyo ilikiukwa na viongozi waliopo madarakani ambao Nipashe, ilipata majina yao ambayo ni Ahmed Issa Mtea,Abas Ramadhani,Yusuph Mohamed,Abdul Azizi Shaban, Masud Hussein,Shaban Juma,Hussein Ijunje,Abdallah Hanafi, Mbaraka Mtonyi, Hassan Waziri na Amini Mussa na hawastahili kuwa viongozi tena.
Hata hivyo Mufti Shekh Simba, aliwataja wanaostahili kuwepo madarakani katika Ofisi ya Mkoa ni Sheikh wa Mkoa, Shaban Juma Abdallah, Kaimu Katibu wa Mkoa, Ustadhi Abdallah Masoud na Mwenyekiti wa halmashauri Ustadhi Mohamed Juma Marawi.
Katika baraza la Masheikh Mkoa ni Sheikh Mwinshehe Mwinyimgeni,Sheikh Nassib Idd Nassib, Sheikh Hussein Said Ijunje,Sheikh Abdallah Hanafi Simba na Sheikh Abdulrahman Salum.
Aliwataja wajumbe wanostahili kuwepo kwenye Halmashauri ya Mkoa ni Hassan Waziri Salum, Said Rashid Golugwa,Athuman Amir Yunus,Seif Juma Banka,Athuman Juma Luwuchu. Mohamed Kidange Laizer, Salim Rajab
Majaaliwa na Rashid Kilavo Msuya.
Ofisi ya Wilaya ni Sheikh abdulrahaman Salum,Ustadhi Mbaraka Musa Mtonyi na ustadhi Mohamed Juma Marawi.
Katika Baraza la Masheikh Wilaya ni Sheikh Shaaban Maarouf,Omar Omar Mgaza, Ayoub Hussein Juma na Hassan Abdallah Mlali.
Aliwataja wajumbe wa halmashauri ya Wilaya ambao wote ni Ustadhi, Ramadhan Abdulrahaman, Mbega Hussin Mbega, Abdallah Yahya Mgongo, Ahamed Mgwasa Twarbushi,Khamis Abdllah Mwalimu,Kiruwa Selemani Kiruwa,Mashaka Abdallahh Said, Wally Juma Laizer, Ibrahim Said Munga na Abdi Nassoro.
Wajumbe wa Mamlaka ya Msikiti Mkuu wa ijumaa Arusha Mjini aliwataja kuwa ni Sheikh Shaaban Juma ambaye ni Imamu na mwenyekiti wa mamlaka,ust. Juma Khamis ni Katibu,Ali Mkuruzi ni Muhazini,Faraji Swai ni Mjumbe, Hassan Magire,Idd Mussa,Said Diria, Ally Idd. Muhamed Ngeseyan, Sheha Mussa, Ahmed Omar, Sheikh Rajab Hassan Kiungiza na
Jawahir Shaha, Maulid Rashid, Rashid Kawapani na Hassan Salum Kikao.
Wengine ni Wazee watano wasuluhishi wa migogoro Msikitini ni Muhammad Abdulrahaman, Ibrahim Said Munga,Kassim Mamboleo,Jaafar Wally na Hussein Bakar.
Viongozi wa Msikiti wa Masjid Quba uliopo mtaa wa Levolosi, aliwataja viongozi wao ni Sheikh Hassan Waziri ambaye ni Imamu na mwenyekiti wa Msikiti, katibu wa msikiti Abubakar Sharif, Mweka hazina Chohan Jumbe na wajumbe ni Ally Shaaban Majeshi, Said Mwinyi,Hassan Msalu,Ghulam Mohamed, Athuman Ndosi,Ramadhan Mdoe,Issa Anzuwani, Hamza Khamis Amiri, Idris Ngido na Yusuph Abdi Ngome.
“Kwa mujibu wa Katiba ya bakwata ya mwaka 199 toleo la mwaka 2008, natamka viongozi halali wa bakwata Mkoa wa Arusha, Wilaya ya Arusha, mamlaka ya msikiti Mkuu wa ijumaa Mjini Arusha na Masjid Quba ni hao nilioorodhesha katika orodha hii niliyosoma,”alisema na kusimama kuondoka.
Naye Mwenyekiti wa Msikiti Mkuu Ijumaa, Abdul Azizi baada ya Mufti kuzungumza na kutaja majina ya viongozi wanaotakiwa kuepo madarakani, alizungumza na waandishi wa habari na kusema Mufti Sheikh Simba amekosea kutaja orodha hiyo wakati suala la uongozi lipo Mahakamani.
“Ila sisi tutaendelea kuongoza Msikitini hadi hapo Mahakama itakapoamua na si vinginevyo, lakini naomba waumini wa dini hii ya Kiislamu wawe wavumilivu mpaka Mahakama itakapoamua, ila alichofanya Mufti Sheikh Simba ni sawa na kuleta vita Arusha,”alisema.
0 comments:
Post a Comment