Mamlaka ya Mapato nchini
imeanzisha mfumo wa kutoa stempu kwa kazi za wasanii ili kudhibiti
unyonywaji wa kazi hizo unaofanywa na baadhi ya wasambazaji na
wazalishaji feki hivyo kuwafanya wasanii wanufaike na kazi zao pamoja na
kulipa kodi kwa serikali.
Akizungumza na Wasanii wa muziki
na filamu jijini Arusha ,Afisa elimu kwa mlipakodi TRA,Frank Mwaselela
amesema kuwa mfumo huo tayari umerasimishwa kisheria na baada ya kutoa
elimu kwa wasambazaji na wasanii hakuna kazi yeyote itakayoruhusiwa
kuuzwa pasipo kuwa na stempu.
Afisa huyo amesema kuwa mfumo
huo utawasaidia wasanii kutoibiwa kazi zao na pia kazi zao kuwa na
ulinzio wa kisheria baada ya kupitia taratibu sahihi ambazo ni
kuzisajili baraza la sanaa (BASATA) Na pia kwa baraza linalohusika na
haki miliki (COSOTA).
Naye Afisa Kodi Msafiri Mbibo
kutoka makao makuu ya TRA amesema kuwa mfumo huo wa stempu umeanza mwaka
jana utasaidia kuondoa wimbi kubwa la wizi na uharibifu wa kazi za
sanaa .
“Mpango huu utasaidia
kuhakikisha kuwa wasanii kuwa mikataba inayozingatia haki za
wasanii,tayari tuimeshaanza kufanya operesheni kuwakamata wanaouza kazi
zisizo na stempu na kuharibu mashione mkoa wa Dar tutaelekea mikoani
pia” Alisema Afisa huyo
Katibu wa Chama cha Wauzaji wa
kazi za wasanii jijini hapa James Male amesema kuwa jitahada
zinazofanywa na TRA na Serikali ni nzuri na ameiomba mamlaka hiyo
kuzitazama kazi walizonunua miaka ya nyuma kabla ya kuanzishwa kwa mfumo
wa stempu.
Mwenyekiti wa Chama cha Wasanii
mkoani Arusha ,Kassim Digega ameipongeza mamlaka hiyo kwa kuonyesha nia
ya dhati ya kulinda kazi zao ili waweze kunufaika na kulinufaisha taifa
kwa kulipa kodi.
Na Mahmoud Ahmad,Arusha.
0 comments:
Post a Comment