“PRESS RELEASE” TAREHE 02.07.2014.
• MTU MMOJA AUAWA KWA KUPIGWA FIMBO KICHWANI NA USONI NA MTOTO WAKE.
• WATU WATANO WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUPATIKANA NA POMBE HARMU YA MOSHI [GONGO]
• JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI RAIA NA WAKAZI WA NCHINI MALAWI KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI KINYUME CHA SHERIA.
• WATU WATANO WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUPATIKANA NA POMBE HARMU YA MOSHI [GONGO]
• JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI RAIA NA WAKAZI WA NCHINI MALAWI KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI KINYUME CHA SHERIA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA
LA MARTHA KYANDO (73) MKAZI WA KIJIJI CHA IBUNGILA AMEUAWA KWA KUPIGWA
FIMBO KICHWANI NA USONI KISHA KUNYONGWA SHINGO NA MTOTO WAKE AITWAE
KISWIGO ANGANISYE (33) MKAZI WA KIJIJI CHA IBUNGILA WILAYANI RUNGWE.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE
01.07.2014 MAJIRA YA SAA 00:30 USIKU KATIKA KITONGOJI CHA MPUNGUTI,
KIJIJI CHA IBUNGILA, KATA YA MALINDO, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA
RUNGWE, MKOA WA MBEYA. AIDHA INADAIWA KUWA KABLA YA KUUAWA MAREHEMU PIA
ALIBAKWA.
INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO NI
BAADA YA MTUHUMIWA AMBAYE INASEMEKANA ANA MATATIZO YA AKILI KUCHUKIA
BAADA YA MAREHEMU KUMPIKIA MAGIMBI BADALA YA UGALI. MTUHUMIWA
AMEKAMATWA.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU WATANO KWA KOSA LA KUPATIKANA NA POMBE HARMU YA
MOSHI. WATUHUMIWA HAO NI PAMOJA NA 1. EMANUEL SAKALA (21) MKAZI WA
MWANJELWA, 2. SHABAN ZUBERI (23) MKAZI WA MWANJELWA 3. JAMES ANDREW (24)
MKAZI WA MAKUNGULU 4. MIKIDADI MWALUGOYA (25) MKAZI WA MWANJELWA 5.
SADIKI HUSSEIN (24) MKAZI WA JUAKALI.
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA WAKIWA
NA GONGO UJAZO WA LITA 5 KATIKA MSAKO ULIOFANYWA KATIKA ENEO LA BENKI –
MWANJELWA, KATA YA IYELA, TARAFA YA IYUNGA, JIJINI MBEYA MNAMO TAREHE
01.07.2014 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI WA POMBE
HIYO, TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
KATIKA MSAKO WA PILI:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU WAWILI RAIA NA WAKAZI WA NCHINI MALAWI KWA KOSA LA
KUINGIA NCHINI BILA KIBALI. WAHAMIAJI HAO HARAMU NI PAMOJA NA 1. THOMAS
JUMA (29) NA 2. BONIFACE CHITETE (29).
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO
TAREHE 01.07.2014 MAJIRA YA SAA 23:15 USIKU KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA
KATIKA ENEO LA KYELA- KATI, KATA YA KYELA-KATI, TARAFA YA UNYAKYUSA,
WILAYA YA KYELA, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA
UHAMIAJI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA WATU WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO
YAO IKIWA NI PAMOJA NA WAHAMIAJI HARAMU ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA
KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment