Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ameandika barua kwenda katika makao makuu ya Simba na juu
ya bahasha kuna kuna jina, Evans Aveva.
Barua hiyo
ya Manji kwa Aveva imetua klabu hapo na kupokelewa na imeelezwa ina ujumbe
mzito ambao umeweka historia katika soka nchini katika kipindi hiki.
Ingawa SALEHJEMBE haijapata kopi ta barua hiyo, lakini imeshuhudia bahasha
hiyo ambayo inakwenda moja kwa moja kwa
Aveva ambaye ni Rais mpya wa Simba.
Aveva
ameibuka na ushindi wa kishindo dhidi ya aliyekuwa mpinzani wake, Andrew Tupa
katika uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita.
Awali SALEHJEMBE ilielezwa barua hiyo ya Manji kwa Aveva ni kuhusu mambo ya siri, hali
ambayo kwa kiasi fulani ilizua hofu kwa baadhi ya mashabiki na wanachama hasa
wa Simba, wakitaka kujua mwenyekiti wa watani wao alikuwa anamweleza nini
mwenyekiti wao mpya.
Lakini
baadaye likapata uhakika kuwa Manji amempongeza Aveva na safu yake yote ya
uongozi kwa kuibuka washindi.
“Barua ile
ya Manji ni pongezi kwa Rais Aveva, tayari ilipokelewa klabuni na kupelekwa
kwake,” kilieleza chanzo.
Manji
ameweka rekodi nyingine kwa kuwa katika siku za hivi karibuni haijawahi kutokea
kiongozi wa klabu hizo kongwe kutoa pongezi na kuutakia kila la heri uongozi
kwa upande mwingine, tena kwa barua.
Taarifa za
ndani ya Simba zinaeleza barua hiyo ya Manji, pamoja na pongezi imesisitiza
Yanga na Simba zinaweza kushirikiana na masuala ya msingi ili kuboresha uwezo wa
kifedha wa timu hiyo.
Lakini Manji
akasisitiza kwamba, Yanga na Simba zitaendelea kupambana uwanjani kwa ushindani
mkubwa kwa lengo la kuinua kiwango cha soka nchini na maslahi ya klabu hizo
kongwe nchini.
0 comments:
Post a Comment