Wednesday, 2 July 2014

LICHA YA ARGENTINA KUTINGA ROBO FAINALI, MESSI AKIRI USWISI `NI HATARII !!!!!!!!!!



Uswizi mmh! Messi, Angel Di Maria na Ezequiel Lavezzi  wakishangilia ushindi kwenye chumba cha kubadilishia nguo.

LIONEL Messi amekiri kuwa Argentina walibanwa sana kabla ya  Angel Di Maria kufunga bao pekee dhidi ya Uswisi  katika dakika za nyongeza lililowapa tiketi ya kwenda robo fainali ya kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
"Wote tulihangaika, tulihangaika na kuhangaika,' alisema Messi. "Tulianza kuwaza kama haitatokea. Lakini mwisho bahati ilituangukia na tunatakiwa kutumia faida hiyo kusonga mbele". 
"Kama ilivyokuwa kwa wote, niliumia sana kwasababu sikufunga. Tulijua kama tungefanya kosa moja tungerudi nyumbani. Hatukutaka kusubiria penati. Tulitaka kumaliza dakika za kawaida".
Big fans: Messi's girlfriend, Antonella Roccuzzo, and their son Thiago watched Argentina's win
Mashabiki bab kubwa!: Mpenzi wa Messi, Antonella Roccuzzo na mtoto wao wa kiume Thiago wakitazama ushindi wa Argentina.
Give this to your dad: Little Messi gets a kiss from his mum in the stands as his dad sets up the winning goal
Mpe busu hili baba yako: Messi mdogo akipata busu kutoka kwa mama yake baada ya baba yake kutengeneza bao la ushindi.
World class: Messi left the Swiss defenders trailing in his wake before laying the pass on for Di Maria

0 comments: